Mabondia wa Afrika ya Kusini Jeffrey Mathebula na Takalani Ndlovu watakutana katika ukumbi wa Carnival City Casino jijini Johannesburg jimbo la Gauteng nchini Afrika ya Kusini katika pambano la mchujo (Elimination Title) la ubingwa wa dunia uzito wa unyoya (Featherweight).
Jeffrey Mathebula (kushoto) na Takalani Ndlovu (kulia) katika moja ya mapambano yao
Wawili hawa ni mahasimu wakubwa wanaojulikana nchini Afrika ya Kusini na walishakutana mara mbili ambapo Ndlovu alishhinda pambano la awali huku Mathebula akishinda pambano la mwisho.
Wakati huo huo mabondia Vusi Malinga wa Afrika ya Kusini na Diarh Gabutan wa Phillipines watakutana katika mpambano mwingine wa mchujo kuwania tiketi ya kukutana na bingwa wa dunia katika uzito wa Bantam.
Promota maarufu wa Afrika ya Kusini Branco Milenkovic wa kampuni ya Branco Boxing Promitions atakuwa ndiye mwandaaji wa mpambano huo utakaofanyika tarehe 23 mwezi wa tatu mwaka huu.
Huu ni mwendelezo wa Shirikisho la Ngumi la kKmataifa IBF katika programu yake ua “Utalii wa Michezo” barani Afrika ambapo imejiwekea lengo la mapambano 100 ya ubingwa mwaka huu.
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.