ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 26, 2013

TAMKO LA WACHUNGAJI KUHUSU WAKRISTU KUCHINJA LAOTA MBAWA MWANZA.

Baadhi ya Maaskofu na wachungaji wa madhehebu ya kikristo mkoani Mwanza leo wameshindwa kutoa tamko juu ya maamuzi ya waziri wa nchi Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu Steven Wassira aliyoyasema juu ya habari ya uchinjaji wanyama, jambo ambalo lilianza baada ya mchungaji kukamatwa akishitakiwa kutokana na malalamiko ya baadhi ya waumini wakislamu kuwa amewalisha kibudu baada ya mchungaji huyo kuchinja mnyama kwenye msiba wa muumini wake huko katika kijiji cha Nyehunge wilayani Sengerema... Pichani ni mmoja wa wachungaji kutoka Nyehunge akihadithia katika kanisa la Anglikana Mwanza lililopo barabara ya posta ya zamani kuelekea Kamanga Ferry na Capripoint..  
Baadhi ya waumini waliojitokeza leo kwenye kanisa la Anglikana jijini Mwanza kusikiliza tamko la baadhi ya maaskofu na wachungaji wa madhehebu ya kikristo wakifuatilia kwa makini maneno yaliyokuwa yakisemwa na mmoja wa wachungaji.
Mchungaji akihubiri kwa kutumia vifungu kadhaa vya Biblia kwenye kusanyiko hilo la Tamko lililofanyika katika kanisa la Anglikana Mwanza, hata hivyo wachungaji hao na maaskofu walishindwa kutimiza adhma ya kutoa tamko juu ya maamuzi ya waziri wa nchi Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu Steven Wassira aliyoyasema juu ya habari ya uchinjaji wanyama.


Viongozi hao wa madhehebu ya makanisa ya Kikristo juzi walipinga maamuzi ya waziri Wassira aliyetinga jijini Mwanza kusuluhisha mgogoro huo, ya Kwamba mwenye haki ya kuchinja ni mwislam kwa nyama ya biashara, kwenye kikao chao leo walichoketi wameshindwa kutoa tamko lao wakipata kigugumizi huku baadhi ya waumini waliofurika kanisani hapo wakipaza sauti zao wakiwatuhumu kuwa wawakilishi wao hao wamehongwa kusitisha utoaji wa tamko hilo.
Baadhi ya wachungaji na maaskofu wakifuatilia yanayojiri ndani ya kanisa.


Baadhi ya wachungaji na maaskofu wakifuatilia yanayojiri ndani ya kanisa, kwa mujibu wa mmoja wa wasemaji wao alitanabaisha kuwa wameahirisha kutoa tamko lao mpaka siku ya jumatatu. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.