ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 26, 2013

"BILA UMOJA VYAMA VYA UPINZANI HAVITAINGIA IKULU KUSHIKA DOLA" ASEMA JUMA DUNI HAJI: CUF KUFANYA MKUTANO KESHO JIJINI MWANZA.

Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni Waziri wa Afya  wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hii leo asubuhi.
 CHAMA cha Wananchi CUF kesho kitafanya Mkutano wake wa hadhara ikiwemo kuwakumbuka wahanga waliofarikidunia kwenye vurugu zilizotokea Zanzibar na jijini Dar es salaam mnamo mwaka 2001 wakitetea haki.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za CUF wilaya ya Nyamagana Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni Waziri wa Afya  wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji alisema kwamba vyama vya siasa vilivyopo nchini havina budi kushirikiana ili kuiondoa CCM madarakani.

"Bila kushirikiana hivi vyama vya upinzani na ikiwa kila kimoja ni kutaka kuingia ikulu kivyake basi itakuwa ni ndoto ya kukiondoa madarakani chama tawala (CCM) ambacho kinashikilia dola" alisema mjumbe huyo. Bofya Play msikilize...

Haji 'Babu' alisema kwamba Chama kinachohamasisha na kuchochea vurugu kitambue kuwa siyo  njia ya kukiwezesha chama hicho cha siasa (Upinzani) kuingia ikulu pia hakitaungwa mkono na wananchi kwani kwa kufanya hivyo wananchi hawatapata ujumbe na sera nzuri wanazopaswa kuzisikiliza kwenya mikutano ya hadahra ili kufanya uamuzi sahihi wa nani wachaguliwe kuwaongoza kupitia chaguzi mbalimbali. 

Hata hivyo ameonya kuwa hatopenda kuona wafuasi wa vyama vingine watakao fika kwenye mkutano huo wa hadhara na kufanya fujo, watambuwe kuwa CUF ni chama makini kilicho na ujasiri wa vurugu lakini kwa sasa hakikusudii kufanya vurugu bali kiko kwaajili ya kuzitangaza sera na mikakati madhubuti ambayo itakiwezesha chama hicho kuungwa mkono kwa kupata wanachama wapya ili kuweza kushinda uchaguzi 2015.

Aidha Chama  cha CUF kimejipanga kujiimarisha zaidi kwa kupata wabunge wengi kwenye uchaguzi ujao nchini ili kuwezesha kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa kama ilivyo Zanzibar.

Juma Duni Haji  ametoa wito kwa wananchi kufika kwa wingi kwenye mkutano huo utakaofanyika katika viwanja vya Nghokozi al-maarufu 'Dampo' vilivyopo barabara ya Uhuru jijini Mwanza.
Sehemu ya wandishi wa habari waliohudhuria kikao cha mazungumzo na Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa.

Na ujumbe ulihusishwa.

Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni Waziri wa Afya  wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hii leo asubuhi.

Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Taifa ambaye pia ni Waziri wa Afya  wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Juma Duni Haji akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza hii leo asubuhi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.