ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 14, 2013

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MWANZA AWAANDALIA HAFLA YA CHAKULA CHA MCHANA MAMALISHE NA WAMACHINGA WA JIJI LA MWANZA

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (kushoto) akiwa ameambatana Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga (katikati) na Mzee Charles Masalakulangwa (kulia)  wakiingia ukumbi wa New Mwanza Hotel kushiriki hafla ya chakula cha pamoja na Mamalishe na Wamachinga wa Mwanza, iliyoandaliwa na Mstahiki Meya .

Meya wa jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula.
"Tumejumuika hapa leo ili kufahamiana zaidi kuweka mikakati na malengo kwa mwaka mpya 2013 lakini pia kuhakikisha kero na matatizo mbalimbali yanayojitokeza ndani ya shughuli zetu na jamii yanashughulikiwa na viongozi wa Serikali ngazi zote husika.." By Mstahiki Meya.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akizungumza na Mamalishe pamoja na wamachinga waliojitokeza jana kushiriki hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Mstahiki meya wa jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani Mhe. Stanslaus Mabula.


Bw. Alfred Wambura ambaye ni mlezi wa Shirika la wamachinga Mwanza (SHIUMA) akitambulisha viongozi wa vitengo mbalimbali ndani ya Shirika la Wamachinga ambalo linajumuisha Mamalishe, Madreva wa pikipiki na Madereva wa Taxi, kwenye hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Mstahiki Meya ndani ya ukumbi wa New Mwanza Hotel. 

Mwenyekiti wa madereva wa pikipiki jijini Mwanza Bw. Makoye akiainisha kwa ufupi majukumu wali yoazimia kuyafanikisha kwa msimu wa Mwaka 2013 wakiwa sehemu ya wamachinga  walioshiriki hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Mstahiki Meya ndani ya ukumbi wa New Mwanza Hotel. 


Sehemu ya kusanyiko la wamachinga na hawa ni madereva wa Taxi.


Sehemu ya wamachinga waliojitokeza ukumbi wa New Mwanza Hotel kushiriki hafla ya chakula cha pamoja na Mstahiki Meya 


Wakisikiliza kwa umakiiini yaliyojiri kabla ya chakula cha pamoja.

Of coz yenye kufurahisha nayo yalikuwepo.


Wamachinga kusanyikoni.


Kisha wamachinga hao wakashiriki chakula cha pamoja.


Kwautaratibu maalum wamachinga walijongea kwenye meza za 'menyu'.


Tukio hili lililoandaliwa na mstahiki meya kwa wadau hawa, upande wao walilitumia pia kama sehemu ya sherehe yao ya kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha 2013. 

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. BRAZA KUMBE NA WEE NI MWANASIASA MBONA SIONI HAPO MACHINGA YEYOTE WA MAKOROBOI, VITUNGUU, SAHARA NA KWINGENEKO JIJINI. KIDUMU CHAMA CHA MAGAMBA CCM. UMETIMIZA UKADA

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.