ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 14, 2013

WANAFUNZI 1,400 WASHINDWA KUINGIA KIDATO CHA KWANZA ILEMELA KWA UHABA WA VYUMBA VYA MADARASA

Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza akizungumza na waandishi wa habari  katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za wilaya hiyo zilizopo Buswelu ilemela jijini Mwanza. 
Wiki moja baada ya kuanza kwa muhula wa kwanza wa masomo kwa mwaka 2013 zaidi ya wanafunzi 1,400 kati ya 6,000 waliofaulu kujiunga kuingia kidato cha kwanza wameshindwa kuanza masomo kutokana na uhaba wa zaidi ya vyumba 24 vya madarasa.

Hilo limebainishwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela  Bi. Amina Masenza wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya wilaya yake kwa msimu wa 2005 hadi 2012 mbele ya waandishi wa habari.

Baada ya kuwepo kwa uhaba huo wa vyumba vya madarasa Halmashauri ya wilaya ya Ilemela imeanza mikakati ya ujenzi wa vyumba hivyo 24 vya madarasa unatarajiwa kukamilika mwezi juni mwaka huu kwa lengo la kuweza kuchukuwa wanafunzi wote walioshindwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari katika kata tisa za Halmashauri hiyo.

Kwa mujibu wa Kaimu Afisa Uchumi wa wilaya Llemela Bw. Philip Nyakutonya amesema kuwa Jumla ya shilingi bilioni 3.2 zimetengwa katika ujenzi wa vyumba hivyo 24 vya madarasa.Bofya Play...

Mkuu wa wilaya alisisitiza kuwa Mkurugenzi wa wilaya yake pamoja na Wataalamu wa Idara ya Elimu kwa kushirikiana na Idara ya Uhandisi tayari wapo katika shule husika kuendelea kusimamia ujenzi wa vyumba hivyo ili uweze kukamilika katika wakati uliopangwa.
Siasa kutoka kwa wanasiasa ni moja kati ya changamoto kubwa inayotajwa kudhorotesha maendeleo ya wilaya ya Ilemela ambapo kumekuwepo na mwitikio hafifu wa wananchi katika mikutano ya hadhara ambayo huitishwa na viongozi na maofisa mbalimbali wa serikali kwaajili ya kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo elimu ambapo kupitia wanasiasa wamekuwa wakichochea wananchi kutochangia maendeleo yao kwa madai kuwa serikali ina fedha za kutosha. Na hapa mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza anatoa ahadi ya kushughulika na watu hao kwa mujibu wa sheria.Bofya Play...

Kaimu afisa elimu Sekondari Kizito Bahati akijibu na kufafanua baadhi ya maswali yaliyowasilishwa na wandishi wa habari wakati wa uwasilishaji taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo wilaya ya Ilemela. 

Sehemu ya wandishi wa habari toka vyombo mbalimbali.
Changamoto nyingine zilizoainishwa:
-Ukosefu wa hospitali ya Manispaa ya wilaya ya Ilemela.
-Manispaa ya Ilemela kutokuwana jengo la Ofisi pamoja na kutokuwa na vitendea kazi (Magari ya watumishi, vifaa vingine vya ofisi, mitambo ya kuzolea taka ngumu na n.k)
-Upungufu wa nyumba za watumishi, waganga katika vituo vya afya na zahanati, manesi, walimu n.k katika Manispaa ya Ilemela pamoja na upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.