ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 29, 2013

MAFUNZO KUHUSU HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KWA WAANDISHI WA HABARI YAFANYIKA LEO MWANZA.


Kamishna Msaidizi wa Tume ya Haki za Binadamu Kanda ya Ziwa Fahamu H. Mtulya, akifungua mafunzo ya haki za binadamu na utawala bora kwa waandishi wa habari jijini Mwanza, yakifanyikakatika ukumbi wa Hoteli Vizano. Msikilize zaidi kwa kubofya Play.

Katika  kutekeleza wajibu huo Tume, imeandaa mafunzo ya haki za binadamu na utawala bora kwa waandishi wa habari katika mikoa saba (7) hapa nchini. Jumla ya waandishi wa habari 112, takribani 16 kutoka kila mkoa wanatarajia kunufaika namafunzo haya.

Mikoa itakayofaidika na mafunzo haya kwaaamu hii ni Mwanza, Tnaga, Lindi, Morogoro, Dodoma na Iringa kwa Tanzania bara na mka wa mjini Magharibi kwa upande wa Zanzibar.
Mwanahabari Imani Hezron wa kituo cha radio City Fm akiwasilisha mchanganuo wa maswali yaliyoulizwa kwa kundi lake kwenye mafunzo kuhusu haki za binadamu na utawala bora kwa waandishi wa habari yanayofanyika hivi sasa jijiniMwanza.

Mafunzo hayo yanalengo la kuongeza uelewa kwawadau vikiwemo vyombo vya habari kuhusu haki za binadamu na utawala bora.

Lengo mahususi la mafunzo haya ni kushirikiana na vyombo hivi katika kueneza na kufikisha elimu za haki za binadamu na utawala bora kwa wananchi ili kujenga jamiiinayoheshimu haki za binadamu na misingi ya utawala bora.
Mwanahabari Mashaka Bartazar wa gazeti la Jambo leo, akiwasilisha mchanganuo wa maswali yaliyoulizwa kwa kundi lake kwenye mafunzo kuhusu haki za binadamu na utawala bora kwa waandishi wa habari yanayofanyika hivi sasa jijiniMwanza.

Waandishiwa habari, wapiga picha na watengenezaji wa vipindi wameaswa kuwa makini katika kuandika na kutoa taarifa mbalimbali kwa umma kwa mtazamo wa kuzingatia haki za binadamu ili kuiepusha jamii kuingia katika mkumbo wa kukiuka haki za binadamu.

Mwanahabari Fortunatus Maneno Sadini wa kituo cha radio SAUT akiwasilisha mchanganuo wa maswali yaliyoulizwa kwa kundi lake kwenye mafunzo kuhusu haki za binadamu na utawala bora kwa waandishi wa habari yanayofanyika hivi sasa jijiniMwanza.

Angalizo limetolewa kwa waandishi kuzingatia masuala muhimu kuviwezesha vyombo vyao vinavyowasilisha taarifa zao kwa umma zinazohusu maamuzi na utekelezaji, kupima taarifa za masuala mbalimbali bila kupuuzia kwani masuala mengine yanaweza kuchangia kushawishi serikali au mamlaka nyingine kufanya maamuzi mbalimbali yasiyosahihi yenye kukiuka haki za binadamu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.