Bondia Charles Mashali kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Adam Ngange wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumb i wa CCM Tandale Dar es salaam jana Mashali alishinda kwa point. |
Bondia Adam Ngange kushoto akioneshana umaili wa kutupiana makonde na Charles Mashali wakati wa mpambano wao uliofanyika kwa mala ya kwanza katika ukumbi wa CCM Tandale Dar es salaam jana. |
Bondia Kalama Nyilawila kushoto akipambana na Athumani Pendeza wakati wa mpambano uliofanyika katika ukumbi wa CCM Tandale Dar es salaam jana Nyilawila alishinda kwa K,o raundi ya tatu |
Baadhi ya wadau wa mchezo wa ngumni wakiwa na mabondia kutoka kushoto ni Kaike Silaju, Nassoro Choro, Selemani Kidunda, Thomas Mashali na Kibavu wakifuatilia masumbwi. |
Bondia Fadhili Majia kushoto akikwepa konde la Antoni Mathias wakati wa mpambano wao uliofanyika CCM Tandale Dar es salaam jana Majia alishinda kwa K,O raundi ya pili. |
Bondia Hassan Mandula kushoto akimlushia makonde James Martini wakati wa mpambano wao uliofanyika jana Mandula alishinda kwa point. picha na www.superedboxingcoach.blogspot.com
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
JANUARI 28, 2013
Rais wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa IBF bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi atakuwa msimamizi mkuu wa mapambano ya ubingwa wa yatakayofanyika nchini Ghana tarehe 8 na 30 March 2013.
Mapambano hayo ni yale yanayowakutanisha mabondia Richard Commey akipambana na Mgana mwenzake Bilal Mohammed wakigombea mkanda wa IBF Afrika na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa Lightweight. Mabondia wote wawili wana rekodi zinazovutia, Commey ana makazi yake katika jiji la London nchini Uingereza.
Mpambano wa pili siku hiyo utawakutanisha mabondia wawili wa Ghana Fredrick Lawson akipambana na bondia machachari Isaac Sowah. Wote wanaishi nchini Ghana.
Mapambano yote yatafanyika wakati bingwa wa dunia wa zamani wa IBF Joseph Agbeko atakapochuana na bondia Luis Melendez wa Mexico kugombea ubingwa wa dunia wa IBO katika uzito wa bantam.
Mpambano mwingine ambao Ngowi atasimamia ni kati ya bondia Helen Joseph wa Nigeria na Fatuma Zarika wa Kenya ambao watagombea mkanda wa IBF wa mabara wa wanawake. Helen Joseph ni mkazi wa Ghana wakati Fatuma Zarika anaishi nchini Ujerumani.
Maofisa wengine watakaomsaidia Ngowi katika mapambano hayo ni pamoja na: Refarii: Rodger Barnor, Jaji namba 1 ni Fred Ghartey, Ghana, Jaji namba 2 ni Confidence Hiagbe na jaji namba 3 ni May Mensah Akakpo, Ghana
Mapambano haya ni kati ya mapambano 100 ambayo IBF imepania kuyafanya katika ukanda wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati mwaka huu 2013.
Imetolewa na:
UTAWALA
International Boxing Federation Africa
Dar-Es-Salaam, Tanzania
|
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.