ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 29, 2013

MTI ULIOKUWA UKINYONGEWA WAAFRIKA WATEKETEA KWA AJALI

Ni ajali iliyotokea majira ya saa kumi jioni ya leo na kusababisha kuvunjika na hatimaye kung'oka kabisa kwa mti wa kumbukumbu, mti ulio tumiwa na Watawala wa Wajerumani enzi za ukoloni kunyongea waafrika, mara baada ya  gari la kampuni ya vinywaji ya  Coca cola lenye namba T988 AFB aina ya TATA kugonga mti huo na dereva wke kukimbia kusikojulikana.

Aidha watu wengine wameligeuza tukio hilo kuwa sehemu ya burudani kuukaribisha mwaka mpya kwa kujiburudisha kwa misoda lukuki iliyokuwemo ndani ya gari hilo huku kukiwa hakuna ulinzi.

Swali je mti huu tutaupata wapi au kumbukumbu yake ndo inapotea...?


Watu wakishangaa ajali ya roli la kubebea soda za kampuni ya Coca cola ya jijini Mwanza kwenye eneo la ajali mara baada ya kuugonga mti wa kihistoria uliokuwa ukitumika kunyongea waafrika enzi za ukoloni nao ukabakizwa mahala hapa ukihifadhiwa kama sehemu ya historia, hatimae umefutika baada ya kugongwa na gari la cocacola na kusambaa wote, eneo la round about ya CCM Mwanza.
Hivi ndivyo ulivyosambaratishwa.

Hivi ndivyo ulivyosambaratishwa hakuna jinsi ya kuurejesha katika hali yake ya kawaida kwani umekuwa kama kulikuwa na mchanja kuni ambaye ameukata vipande vipande vidogo vidogo, wadau wengi wameshauri liwekwe jiwe la msingi au mnara mahala hapa kama kumbukumbu.
 MAJUZI.
Mwonekano wa awali wa mti huo kabla ya ajali hiyo ulihamasisha moja kati ya vipindi Clouds Tv (Siz Kitaa) kufanya kipindi eneo hili la kumbukumbu.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. MWENYE KAMPUNI AGALAMIKE AJENE MNARA WENYE KUFANANA NA MTI HUO
    MISSANA DHL BUKOBA

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.