ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 27, 2012

TBL YATUMIA ZAIDI YA SHILINGI MILLIONI 30 KUTEKELEZA MRADI UPANDAJI MITI

Ofisa Misitu na Mazingira Mkoa wa Mwanza, Henry Mongi.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imetumia zaidi ya Shilingi milioni 30 kutekeleza mradi wa upandaji miti ili kulinda vyanzo vya maji kuboresha na kutunza mazingira nchini katika kipindi cha mwaka jana na mwaka huu.


Kauli  hiyo imetolewa na mkurugenzi wa uhusiano na Jamii na Sheria wa TBL. Stephen Kilindo, wakati wa kazi ya upandaji miti iliyofanywa na wafanyakazi wa kampuni hiyo majuzi hapa jijini Mwanza.
Wafanyakazi hao wa TBL walipanda miti katika barabara za Kenyata, Balewa, Machemba, Shule za Nyamagana na Nyegezi, Uwanja wa Furahisha na eneo la kiwanda cha TBL, Mwanza.

Kilindo alisema TBL kupanda miti ni kuikumbusha na kuihamasisha jamii kutilia mkazo kuona umuhimu wa kutunza mazingira na kulinda vyanzo vya maji kwa faida ya vizazi vijavyo, lakini pia kukabiliana nachangamoto za mabadiliko ya tabia nchi na madhara yake.

Akizindua mradi huo kwa niaba ya Mkuu wa mkoa, Mhandisi Evarist Ndikilo, Ofisa Misitu na Mazingira Mkoa wa Mwanza, Henry Mongi alisema watumishi wa kada mbalimbali wa sekta za umma na binafsi hawana budi kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kulinda, kutunza na kuboresha mazingira.
Mgeni rasmi Henry Mongi akipanda mti kama ishara ya kuzindua kampeni hiyo jijini Mwanza.


Zoezi la wana TBL likiendelea.

Wadau wa TBL wakiongozwa na Mr. Erick (kulia kabisa mwenye karatasi ya ramani) pamoja na viongozi wengine wa kada mbalimbali wakijadili jinsi ya kufanikisha kampeni ya upandaji miti iliyoasisiwa na TBL kanda ya ziwa.

Meneja Rasilimali watu TBL Mwanza Bi. Ester Masala akipanda moja kati ya miti 2600 iliyopandwa jijini Mwanza kwenye kampeni maalum iliyosimamiwa na kampuni ya bia nchini TBL.

TBL

TBL na mikakati ya utunzaji mazingira hapa ni katika eneo la shule ya sekondari Nyegezi jijini Mwanza.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Nyegezi nao wakishiriki mchakato huo wa upandaji miti ambapo jumla ya miti 2600 imepandwa jijini hapa kupitia kampuni ya TBL.

Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Nyegezi akisoma lisala ya shukurani kwa kampuni ya TBL kufanikisha zoezi la upandaji miti na uhamasishaji wa kutunza mazingira.

Ni sehemu ya timu ya wafanyakazi wa kampuni ya kutengeneza bia nchini TBL ya jijini Mwanza wakiwa wameketi kumsikiliza mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Nyegezi mara baada ya kukamilisha zoezi la upandaji miti iliyofanywa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwenye mazingira ya shule hiyo.

Mkurugenzi wa uhusiano na Jamii na Sheria wa TBL. Stephen Kilindo, akitoa ufafanuzi wakati wa kazi ya upandaji miti iliyofanywa na wafanyakazi wa kampuni hiyo majuzi hapa jijini Mwanza. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Diwani wa kata ya Mkuyuni Lugo Fasheni, Ofisa Misitu na Mazingira Mkoa wa Mwanza, Henry Mongi na Kaombwe Phidelis.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.