ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 27, 2012

MH. LAMECK AIRO NA MIKAKATI YAKE KUKUZA ELIMU JIMBO LA RORYA.

Mbunge wa Rorya Lameck Airo akifanya uzinduzi rasmi wa shule ya msingi kata ya Kirogo yenye madarasa mawili tu huku mengine mapya yakiendelea kujengwa kwa nguvu ya wananchi pamoja na sapoti ya mbunge huyo kama sehemu ya kusapoti maendeleo ya elimu wilaya ya Rorya mkoani Mara. 

Hatua yapili kuelekea kuona kibao cha uzinduzi. 

Hatua hii nifaraja kwa wananchi wa kata ya Kirogo kwani ni safari kuelekea kuisaka elimu bora yenye manufaa kwa watoto waishio maeneo ya karibu katani humu.

Jiwe la msingi la jengo hili limewekwa na Mhe. Lameck Airo Mbunge wa Wilaya ya Rorya tarehe 21/12/2012.

Uhaba wa madawati katika shule nyingi za msingi na sekondari nchini umeendelea kuumiza vichwa vya wengi wapenda elimu pamoja na wazazi kwa ujumla hali iliyomlazimu mbunge Lameck Airo kujisukuma kuchangia madawati kama inavyoonekana pichani ndani ya moja ya madarasa haya.

Mara baada ya kufanya ufunguzi kwa shule hiyo Mhe. Mbunge Lameck Airo alizungumza na wananchi wa kata hiyo kuweka msisitizo kwa masuala kadhaa ikiwemo matunzo ya majengo ya shule, ukarabati wa kila mara, kuhamasisha elimu na uboreshaji wa michezo.

Wananchi wa kata ya kirogo wakimsikiliza kwa umakini Mbunge wao kwenye kusanyikohilo.

Mzee kiongozi wa kata hiyo akimkabidhi Mhe. Mbunge Lameck Airo zawadi ya kuku dume (Jogoo) kuafiki mchango wake katika maendeleo ya kata ya Kirogo. 

Mmoja wa akinamama wa kata ya Kirogo akijidai na vazi lake kusanyikoni.

Katika kuchangia na kuendeleza michezo ndani ya kata ya Kirogo Mbunge wa Rorya Mhe. Lameck Airo aliikabidhi mipira kwa Captein wa timu ya Cheleche Fc George Fabian (kushoto) kama hamasa kwa timu hiyo iliyo moja ya timu zinazofanya vizuri katika uwakilishaji kata hiyo kwenye kandanda.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.