ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 4, 2012

SHAMRASHAMRA ZA LALA SALAMA NDANI YA BIAFRA KINONDONI LEO, TUKIELEKEA KWENYE KILELE CHA SERENGETI fiesta 2012

Moja ya bango yaliyosambaa kila koja ya jiji la dar na kwingineko kuhusiana na ujio mkubwa wa Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani,Rick Ross atakaetumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,litakalofanyika siku ya jumamosi,Oktoba 6 katika viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar Es salaam,Tamasha hilo pia litawahusisha wasanii mbali mbali wa hapa Tanzania.

Ujumbe maridhawa wa kinywaji maalumu cha tamasha la Fiesta.

Mdau akiwa amepozi ni fulana yake ya fiesta mara baada ya kukabidhiwa na mwanadada Antu Mandoza ambaye ni mmoja wa watangazaji wa Clouds TV,wakiwa ndani ya viwanja vya Biafra mapema leo Kinondoni kwenye kuelekea kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012.

" Hii ndio ya kwangu,ntaitinga kwa ajili ya kumuona Rozzzaaaay".!

" Daah hii inanitosha kabisa"!

Mtangazaji wa Clouds TV,Mussa Husein akizungumza na mmoja wa mashabiki wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ndani ya viwanja vya Biafra mapema leo jioni wakati skwadi zima la lala salama kwenye kuelekea kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012 viwanjani hapo

Antu Mandoza akishoo love na baadhi ya mashabiki

Ni kushoo love tuu afuu Bhaaaaassss....!

Mussa Huseini pichani kati akiwa amezungukwa na Mashabiki/wapenzi wa tamasha la Serengeti Fiesta wakiwa wamejitokeza kwa wingi leo kwenye viwanja vya Biafra,wakati skwadi zima la lala salama kwenye kuelekea kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lilipotinga kwenye viwanja hivyo na kutoa zawadi mbalimbali kwa washabiki hao,ikiwemo fedha taslim,simu,tiketi za kuingilia kwenye tamasha hilo pamoja na fulana.

Mashabiki na wapenzi wa tamasha la Serengeti Fiesta wakiwa wamemzunguka kwa wingi mtangazaji Clouds FM,Dj Fetty leo kwenye viwanja vya Biafra,wakati  skwadi zima la lala salama kwenye kuelekea kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012 lilipotinga ndani ya viwanja hivyo na kutoa zawadi kem kem kem kwa washabiki hao,ikiwemo fedha taslim,simu,tiketi za kuingilia kwenye tamasha hilo pamoja na fulana.

Kama ada sehemu yenye mkusanyiko tunapeana riziki hivyo hivyo kwa namna moja ama nyingine masiha yanaendelea.

Mratibu wa kikosi cha lala salama kuelekea kwenye kilele cha tamasha hilo hapo jumamosi,Mully B akitoa maelekezo mafupi kwa baadhi ya watu waliojishindia tiketi za fiesta.

Mtangazaji wa Clouds FM,Dj Fetty akifanya mazungumzo ya mmoja wa washindi aliyejishindia simu mapema leo jioni kwenye viwanja vya Biafra,Kinondoni jijini Dar.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.