ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 28, 2012

ROCK CITY MARATHON YAFANA

Mashindano ya Rock City Marathon yamechukuwa kasi hii leo jijini Mwanza na kumalizika kwa msisimko wa aina yake ambapo mwisho wa mashindano washindi walizadiwa stahiki zao.

Mashindano hayo yameshirikisha wakimbiaji kutoka mataifa zaidi ya 10 wakiwemo wenyeji Tanzania, ambapo mbio zilizohusishwa ni za 2 kwa watoto, kilomita 5 mtu yoyote, kilomita 3 walemavu, kilomita 3 wazee na kilomita 21 zote kila moja zikihusisha wanaume na wanawake. 


Kumbukumbu muhimu.....
Kwa upande wa watoto wao walishiriki mbio za kilomita 2, pichani wakianza mbio hizo kwenye eneo la barabara ya Mwaloni karibu na Azania Bank ambapo walimaliza mbio hizo uwanja wa CCM Kirumba.
Baba akimpa sapoti mwanae kumaliza mbio za Rock City marathon kilomita 2 leo asubuhi.


Siyo mchezo....Yahitaji moyo..

Mshindi wa kwanza Mwita Kopiro Marwa kutoka Mwanza akimaliza mbio za Rock City Marathon kilomita 21 wanaume ndani ya uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.


Mshindi wa kwanza  wanawake mbio za kilomita 21, Mary Naaly kutoka Arusha akivuka mstari wa ushindi.


Mbio zilizovuta macho na masikio ya wengi ni zile ndefu za kilomita 21 ambapo kwa upande wa wanaume mshindi wa kwanza ni Mwita Kopiro Marwa kutoka Mwanza aliyejishindia medali ya dhahabu na kitita cha shilingi milioni 1 na laki 2, mshindi wa pili ni Joseph Chacha kutoka mkoani Mara aliyejishindia medali ya fedha na kitita cha shilingi laki 9, huku mshindi wa tatu akiwa ni Alphonce kutoka Arusha aliyejishindia medali ya shaba na shilingi laki 7.

Kwa Upande wa wanawake mshidi wa kwanza ni Mary Naaly kutoka Arusha, wa pili ni Sara Ramadhani wa Zanzibar na watatu ni Anastazia Msandai kutoka Arusha ambapo zawadi zao zilikuwa ni sawa na zile za wanaume tulizozitaja.

Pascal Emanuel ameibuka kuwa mshindi wa kwanza Rock City Marathon kwa upande wa walemavu akikimbia kilomita 3. 



Upande wa wazee wanawake Mungulo Lubisi kutoka Bariadi ameibuka mshindi nafasi ya kwanza ile hali kwa upande wa wanaume mshindi ni Selemani Kishuzi ambaye ni mwalimu wa Mwanza Sekondari na hapa anaelezea siri ya mafanikio... 


Mshindi kwa mbio za kilomita 2 watoto upande wa wavulana Iddy Suguta kutoka mkoani Mara akiwa na medali yake ya dhahabu pamoja na fedha kwenye bahasha.


Viongozi, wafanyabiashara na watu wenye uwezo nchini kuachana na tabia ya kuvamia maeneo maalum yaliyotengwa kwaajili ya michezo ili vipaji vinavyochipukia husussani vijana na watoto viweze kupata nafasi ya kujiendeleza.

Wito huo umetolewa leo na rais wa Chama cha riadha nchini Anthony Mtaka wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Mwanza kwenye hitimisho la mbio za Rock City Marathon kama sehemu ya tathimini yake kwa michuano hiyo..

Jane Matinde ambaye ni Afisa uhusiano wa Airtel amewashukuru wakazi wa Mwanza kwa kujitokeza kwenye michuano hiyo sambamba na kuweka bayana mpango ya siku za usoni ya Airtel katika kuendeleza na kukuza michezo mbalimbali hapa nchini.. Msikilize kwa kubofya play hapo juu..
Time kushow love kutoka kushoto Kalama Mura, Baby Madaha, Jackob Markus na Sir Juma Nature.
Mwanamuziki toka Bongo Fleva Baby Madaha akitoa burudani kwa wakazi wa jiji la Mwanza waliohudhuria mashindano ya Rock City marathon kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Hapa Sir Juma Nature, Kara Mura na Baby Madaha walishirikiana kupitia wimbo mpya ambao soon utausikia kwa redio zetu na kutoa burudani kwa wakazi wa jiji la Mwanza waliohudhuria mashindano ya Rock City marathon kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Ingawa kulikuwa na mvua ya hapa na pale haikusababisha mashabiki kukwepa kuikaribia burudani iliyokuwa ikiririka jukwaani.

Hawa ndio wadhamini wa Rock City Marathon 2012.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.