Mmoja kati ya wadau wa michezo la jiji la Mwanza ambaye amekuwa akichangia maendeleo ya soka mkoani humo John Kadutu pamoja na kwamba amejitokeza kuwa mgombe pekee wa nafasi ya kuwa Mjumbe atakaye wakilisha vilabu vya mpira wa miguu mkoa wa Mwanza amewataka wajumbe kutumia busara wakati wa kupiga kura na kumpa kura zote za ndiyo...
Naye katibu wa Chama cha soka wilaya ya ilemela Juma Msaka akliyejitosa kuwania nafasi ya Katibu wa Chama Cha Mpira Mkoa wa Mwanza, sera yake imekuja na Kauli mbiu ya 'Kutanua na kuendeleza soka mkoa wa Mwanza'Mgombea wa mwisho kwa siku ya leo aliyejitokeza kujinadi huku wengine bado wakitafakari jinsi ya kunadi sera zao ni Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa timu za Toto Africans, Cop United na Pamba zote za Mwanza.
Si mwingine bali ni Katibu wa Chama cha soka wilaya ya nyamagana Munga Lupindo ambaye anagombea nafasi ya Ujumbe kamati tendaji ya Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mwanza
Tupe maoni yako
John Kadutu namkubali sana kama atapitishwa kama mwakilishi wa vilabu.
ReplyDeleteHuyu jamaa ni mpambanaji hakuna mfano na Mwanza tutakuwa tumepata mjumbe asiye weza kukubali kuona maslahi ya Mwanza yanachezewa na TFF