ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 24, 2012

KILIMAHEWA IMESAHAULIKA MIUNDOMBINU YA BARABARA

Katapila likisawazisha barabara mbadala eneo la kata ya Kilimahewa jijini Mwanza ili kupisha ujenzi wa daraja unaoendelea kwa njia ielekeayo Kiloleli, Nyasaka, na kuunganisha hadi barabara mpya ya Nyakato.

Ukarabati huu unaendelea kwa kusuasua ingawa juhudi za wanasiasa zinafanyika kuhimiza uharaka.

Katika daraja la Big Bite ambako ujenzi unaendelea mabari hayana njia ya kupita zaidi ya watu kujipenyeza pembezoni na kuvuka kwenye ki-ki-kijidaraja. 

Ujenzi wa daraja hili unachamngamoto nyingi sana mojawapo ni chemchem ya maji.

Sina uhakika kama vifaa vya ujenzi kwa daraja hili linalohitaji nguvu ya ziada kama vinatosha kwani uondoshaji wa maji unafanywa kwa kutumia ndoo badala ya pump ya kufyonza maji.

Muonekano wa daraja.

Msamaria mwema akimvusha kikongwe kwenye ki-ki-kijidaraja kilichotengenezwa kwa wavukao kwa miguu 

Kwa ukaribu zaidi kijidaraja hicho kisichosalama.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.