ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 3, 2012

UCHUNGUZI WA AWALI: WAUAJI WA MWANDISHI DAUD MWANGOSI NI HAWA

Taarifa zasema kuwa huyu askari aliyeelekeza mtutu tumboni ndiye aliye msambaratisha marehemu kwa BOMU LA MACHOZI mbalo ndilo lilimtoa uhai wake. 
Tukio hili linatajwa kutendeka mbele ya kiongozi wao hapa ni gari la lake likiwa jirani wakati wakimbeba mwenzao angalia pembeni ni shangingi la kiongozi wao.
Lakini kwa vile hawakuwa makini hata wao ukaribu huo wa kulipua BOMU LA MACHOZI ulisababisha madhara kwa askari wao kuumia, na huyu ni miongoni mwa wale waliokuwa wamemshikilia marehemu. Angalia hapo wamemaliza kazi, wanamwondoa mwenzao na kuuacha mwili wa mwandishi mpendwa wetu DAUD MWANGOSI nyuma yao.

HABARI KWA UFUPI KWA MSAADA WA GAZETI LA MWANANCHI 
Mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daud Mwangosi anadaiwa kuuawa kwa bomu lililorushwa na polisi katika vurugu hizo.

Awali, inadaiwa kuwa mwandishi huyo alishambuliwa kwa marungu na Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kabla ya bomu hilo kumjeruhi vibaya tumboni na kusababisha kifo chake.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio, alisema wakati mwandishi huyo akishambuliwa na polisi, mmoja wa askari wa jeshi hilo aliwazuia wenzake kuendelea kumpiga akiwaeleza kuwa anamfahamu kuwa ni mwandishi wa habari, huku akimkumbatia.

Shuhuda huyo alidai kwamba jitihada za askari huyo hazikusaidia, kwani baada ya kutupwa kwa bomu hilo lililosababisha utumbo wa mwandishi huyo kutoka nje, polisi huyo naye alijeruhiwa mguu.

Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso alikana polisi kumuua mwandishi huyo akidai kwamba kilichosababisha kifo chake ni kitu kilichorushwa na wananchi ambapo alisema polisi inakichunguza. “Mwandishi alikuwa akikimbia kutoka upande wa wananchi kuelekea walipokuwa polisi. Kuna kitu kilirushwa kikitokea upande wa wananchi na kumfikia ambacho kilimjeruhi pia askari akiwamo Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS).” Hata hivyo, hakumtaja OCS huyo.

Vurugu hizo ziliibuka baada ya polisi kufika Nyororo na kuwataka viongozi wa Chadema pamoja na wafuasi wao kutawanyika kwa kuwa walikuwa hawaruhusiwi kufanya mkusanyiko wowote kutokana na amri iliyotolewa na jeshi hilo awali.

Polisi mkoani Iringa jana asubuhi walilipiga marufuku kufanyika kwa maandamano na mikutano yote ya halaiki ya kisiasa mpaka hapo Sensa ya Watu na Makazi itakapokamilika baada ya kuongezwa wiki zaidi.

Hata hivyo, pamoja na amri hiyo Chadema kilifanya mkutano wilayani Mufindi kitendo ambacho polisi walisema ni kinyume cha sheria.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda alisema ambaye alikuwa akiongoza askari wake kuwatawanya wafuasi wa Chadema katika eneo hilo, alisema kazi yao ilikuwa ni kutekeleza amri akisema wao si wanasiasa. “Nataka watu wote mtawanyike,” alisema Kamanda Kamuhanda.
Hata hivyo, viongozi wa Chadema walikaidi amri hiyo wakisema kuwa walikuwa wanaendelea na mikutano yao ya ndani siyo ya hadhara, kauli ambayo polisi walikataa.

Kabla ya polisi kutaka kuwakamata viongozi hao, wananchi waliwazuia kufanya hivyo na hapo ndipo vurugu zilipoanza na mabomu ya machozi kupigwa kitu na kila mtu kutawanyika.
Katika vurugu hizo Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Hamad Yusuf alikamatwa na mtu mwingine ambaye jina lake bado halijafahamika.

Jukwaa la Wahariri latoa tamko
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Nevile Meena amesema jukwaa linalaani kitendo cha polisi kuua mwandishi kwa sababu za kisiasa.
“Tunalaani sana kitendo kilichofanywa na polisi kuua mwanahabari kwa sababu za kisiasa.”

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. Jamani kusoma hatujui hata picha hatuoni kweli hicho kitu kilichotupwa na mwananchi wapi na wapi hebu tuwe wa kweli angalau kidogo tuu, Poleni sana wanahabari wa Iringa, Tanzania na Dunia nzima kwa kumpoteza Daudi Mwangosi, Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahala pema peponi. Amina

    ReplyDelete
  2. Hawa ni polisi wauaji, siku zote watu wanajua mauwaji yao wanayofanyia watu wasio na hatia lakina serikali kandamizi iko kimya.Dhuluma hii imefikia katika kiwango cha juu sana.Wakuu wa polisi wako kimya kwa maslahi yao binafsi lakina wajue ya kuwa wamo katika khasara kubwa. Mwisho wa viongozi dhalimu UMEFIKA.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.