ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 12, 2012

TUSITEGEMEE WAWEKEZAJI KWA KILA JAMBO



Watoto wakifurahia madawati kwa shule yao ikiwa ni moja ya shule zinazozunguka mgodi wa ABG North Mara zilizonufaika na msaada huo.

Madawati

Haya ndiyo maisha ya wanafunzi kabla ya msaada wa madawati .

Kutokana na ukosefu wa madawati ni wanafunzi wachache tena wa kuhesabu ndiyo hukaa kwenye viti wanaobaki  wote hukaa sakafuni.

Baiskeli za Magurudumu matatu kwa watu watatu wasiojiweza pia zilitolewa.

Wadhamini.
Augustine Mgendi: TARIME
SERIKALI imesema kuwa kamwe haiwezi kumtegemea mwekezaji  kwa kila kitu huku baadhi ya Mambo yanaweza kufanywa na wanajamiii wenyewe katika sehemu huska.
 
Kauli hiyo ya Serikali ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bw John Henjewele katika hafla ya kukabidhi Madawati kwa baadhi ya shule zinazozunguka mgodi wa ABG North Mara, Vifaa vya Shule kwa baadhi ya wanafunzi na baiskeli ya Magurudumu matatu kwa watu watatu wasiojiweza.
 
Alisema kuwa pamoja na Misaada inayotolewa na Mgodi huo kwa Jamii lakini pia serikali inashukuru Mahusiano Mazuri yaliyopo katika Mgodi huo wa ABG North Mara na Jamii.
 
Mkuu wa Wilaya huyo aliushukuru Mgodi huo kwa kugundua hali ya Walemavu,kutoa vifaa vya Elimu huku akisema hiyo ni hatua moja mbele katika kuisaidia Jamii.
 
 “Kwanza tushukuru sana Mahusiano yaliyopo kati ya Mgodi huu na Jamii lakini pia hatuwezi kumtegemea Mwekezaji kwa kila Jambo lazima sisi wenyewe tujitoe katika kufanikisha baadhi ya Mambo yetu” alisema Mkuu huyo wa wilaya.
 
Akimkaribisha Mkuu huyo wa Wilaya Meneja mkuu wa Mgodi wa North Mara Bw Gary Chapman,alisema Mgodi huo ni miongoni mwa Migodi Afrika ambayo imekuwa ikiwekeza katika Jamii hasa katika suala la Elimu,Afya,Maji na Maendeleo katika Jamii.
 
Alisema Pamoja na kutotimiza mahitaji kwa shule za Sekondary kwa asilimia mia lakini watajitahidi kushirikiana na Jamii jiyo katika kujiletea Maendeleo.
 
 “Mgodi huu ni moja ya Mgodi Afrika ambao unajitolea katika kusaidia Jamii hasa katika Elimu,afya,maji na Masuala la Maendeleo,lakini pamoja na kutotimiza Mahitaji ya Jamii kwa asilimia kubwa bado tutaendelea kushirikia na nao” alisema Bw Gary Chapman
 
Aidha Uongozi wa Mgodi huo umetoa Madawati zaidi ya 1000 kwa shule za Nyangoto na Matare zilizopo katika eneo la Nyamongo wilayani Tarime Mkoani Mara huku Miradi yote Mitatu ya Elimu,msaada ya Baiskel na Madawati hayo ikigharimu kiasi cha shilingi milioni 188.
 
Watu waliopewa Baiskel hizo za Miguu mitatu ni pamoja na  Eliza Mwikwabe ambaye ni mfanyabiashara ndogondogo,Penina Mseti muuza mboga na Nyanya pamoja na Gesongo Chacha ambaye ni fundi wa kuchomelea vyuma.
 
Awali akisema Risala kwa Mgeni Rasmi Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Nyangoto Bw Ghati Keraryo alisema kuwa shule zote mbili za Nyangoto na Matare  zina jumla ya Madawati 202 kati ya 654 ambayo yanahitajika.

Alisema kwa niaba ya Walimu wa shule hizo wanapenda kutoa shukurani kwa Mgodi wa ABG North Mara kwa kutambua Umuhimu wa Changamoto moja wapo zinazokabili shule hizo ikizingatiwa kwamba shule hizo zipo karibu na Mgodi huo.
 
Mbali na Msaada huo wa Madawati kwa shule hizo,Msoma risala huyo alisema kuwa  bado shule hizo zina upungufu wa Viti 46 na meza 18,huku akiuomba Mgodi huo kuendelea kujenga Shule hizo kama Mkataba ulivyoainisha katika ya Kijiji na Mgodi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.