ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 25, 2012

BREAKING NEWS: CHADEMA WILAYA YA ILEMELA YAZIDI KUGUBIKWA NA VURUGU, SLAA AKWEA PIPA FASTA KUNUSURU.

HALI NDANI YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)WILAYA YA ILEMELA YAZIDI KUGUBIKWA NA VURUGU NI KATIKA KUWAPATA WAGOMBEA WA NAFASI YA MEYA NA NAIBU MEYA MANISPAA YA ILEMELA.

Na  ALBERT G. SENGO
BAADA ya kutokea vurugu ndani ya Chama cha CHADEMA wakati wakifanya uchaguzi wa wagombea wa nafasi ya Meya na Naibu Meya mwishoni mwa wiki (Jumapili 23sept 2012) kwa kukaidi Hati iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza na Jaji Sumar iliyozuia chama hicho kuendelea na mchakato wa uchaguzi huo hadi hapo uamuzi wa kesi ya mwanachama wake iliyofunguliwa itakapotolewa uamuzi baada ya kupingwa kuvuliwa uanachama na Kamati Kuu ya CHADEMA hivi karibuni.

Habari za uhakika kutoka ndani ya chama hicho zimeeleza kwamba baada ya vurugu kubwa zilizotokea katika ukumbi wa Hoteli ya Ladson iliyopo Wilayani Ilemela Jumapili majira ya saa 6:42 mchana na badae Kamati ya Utendaji ilikaa majira ya jioni na kufanikiwa kufanya kikao cha kuwachagua wagombea wa nafasi ya Meya na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilemela na kuwapata wagombea waliopigiwa kura na wajumbe halali wa kamati hiyo.

Kufuatia mchakato huo hali imegeuka baada ya Mbunge wa Jimbo hilo Haghness Kiwia kutishia kujiuzuru ujumbe wa Kamati hiyo kwa vile waliochaguliwa walikuwa si chaguo lake kwani waliopitishwa ni Madiwani wa Jinsia ya Kike, na hakubaliani nao, akiiangushia lawama Kamati ya uchaguzi.

Waliochaguliwa ni Mhe.Marietha Chenyenge (diwani kata ya Ilemela) nafasi ya Meya na Mhe.Rose Brown (diwani kata ya Pasiansi) nafasi ya Naibu Meya.

Wagombea waliopigwa chini katika uchaguzi huo wa Jumapili usiku ni Mhe. Dani Kahungu (diwani kata ya Kirumba) nafasi ya Meya na Mhe.Abubakar Kapera (diwani kata ya Nyamanoro) Naibu Meya, hali ambayo iliufanya uongozi wa juu wa chama hicho kumtuma mwakilishi wa Katibu Mkuu wa wake ambaye ni Katibu wa Oganaizesheni na Mafunzo Benson Kigaila, kuja Wilayani humo na kutoa taarifa na msimamo wa Makao makuu juu ya majina yaliyopendekezwa ya wagombea na kutenguliwa walioshinda.

Hatua ya mwakilishi huyo kukutana na Madiwani wa CHADEMA na kuwaeleza taarifa hizo za makao makuu ilionekana kupingwa na baadhi ya madiwani walio wengi akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo Highness Kiwia na hali haikuwa salama na kilichotokea ni kuanza kuvurumishiana makombora ya maneno yasiyofa na kusema uamuzi huo ni wakidikteta unaofanywa na uongozi huo wa juu wa chama hicho.

“Hali ilikuwa mbaya sana kwa Kagaila baada ya kuwaelezea madiwani taarifa ya maelekezo ya makao makuu imeonyesha jinsia ndani ya CHADEMA haina haki na thamani hivyo ni uamuzi ambao hatukubaliani nao na kama ni wa kutushinikiza basi hatuko tayari kwa hili na tutafanya maamuzi ambayo pia yatakigharimu chama kwa vile wanachokifanya si sawa na wameshindwa kuheshimu maamuzi ya Kamati ya utendaji ya wilaya iliyopewa jukumu hilo kikatiba” Alisema diwani mmoja.

Aliongeza kuwa hata baada ya mwakilishi huyo aliyeagizwa toka makao makuu kukutana na Kamati ya utendaji wilaya hali iliendelea kuwa tete na kuzuka mvurugano kwa baadhi ya wajumbe na wanachama kutaka kuzichapa kavu kavu ambapo Mwita Hillside na Nyarapa Hatari walimshambulia Katibu Mwenezi Carlos Majura wakipinga kumtetea Kagaila.

Hadi tunatundika taarifa hii bloguni, Kamati ya Utendaji Wilaya ya Ilemela imekataa kukubaliana na uamuzi huo wa CHADEMA makao makuu huku baadhi ya madiwani wakidai kumuunga mkono mgombea aliyeenguliwa kwa madai ya kuvuliwa uanachama Mhe. Henry Matata(diwani kata ya Kitangili) ambaye amekimbilia Mahakamani kupinga maamuzi yaliyofanyika juu yake.

Taarifa za uhakika zimeeleza kuwa baada ya mwakilishi huyo kutoa taarifa makao makuu juu ya kimbembe cha kukataliwa mapendekezo yaliyotolewa na uongozi ngazi ya juu, Imepelekea katibu mkuu wake Taifa Dkt. Wilbroad Slaa kufunga safari jioni hii kutinga jijini Mwanza ili kunusuru mpasuko uliojitokeza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.