ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 26, 2012

USIKILIZE MUUNGANO WA MACHINGA MWANZA KUHUSU KUZOMEWA KWA PINDA

Uongozi wa Muungano wa Wamachinga jiji la Mwanza umejitokeza hadharani na kulaani tukio la hivi karibuni linalosadikiwa kufanywa na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Nyamagana ambapo walimzomea Waziri Mkuu Bw.Mizengo Pinda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Sahara 17/09/2012.
Muungano huo umesema kuwa haukuona vyema kukaa kimya mara baada ya tukio hilo la udhalilishaji kufanyika hivyo ukaamua kukutana na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Bw. Baraka Kondisaga na kuwasilisha kauli yao wakisisitiza kuwa fujo zote zilizofanyika Sahara, ni  fujo zilizoandaliwa na wahuni na si wamachinga kama inavyotajwa hivyo wao wanazikemea na kuzilaani kwa kauli moja wakisema kuwa hawahusiki na kuiomba serikali kuwachukulia hatua za kisheria wale wote walio husika.

Muungano huo uko tayari kushirikiana na serikali kuwabaini na kuwakamata wale wote waliohusika na rabsha zilizotokea Sahara kwani ule ulikuwa mkutano wa kiserikali na muda adhimu kwa wananchi kama kundi lao (Wamachinga) kuuliza maswali kutoa kero zao zenye ufumbuzi wa papo kwa papo au ufumbuzi wa muda.  

Umoja huo umemwomba Waziri Mkuu Mh. Pinda kutokata tamaa kurejea kwa mara nyingine mkoa Mwanza kufanya mkutano kama huo.

Wakiingia kwenye ukumbi wa Ghand kwaajili ya kuongea na mkuu wa wilaya ya Nyamagana Bw. Baraka Kondisaga (Mtumishi wa Mungu)

Sikiliza alichosema Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Bw. Baraka Kondisaga kwa kubofya play...
Kusanyiko.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.