Vijana wengi wamejitokeza katika tukio hili la kijamii lililoasisiwana jeshi la polisi nchini. |
Vijana wachezao soka toka mitaa mbalimbali ya wilaya ya Ilemela wamejitokeza kushiriki michuano hiyo. |
Maandamano hayo hatimaye yaliwasili katika dimba la CCM Kirumba na kupokewa na mgeni rasmi wa Michuano hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Amina Masenza. |
Mchezo wa kwanza kwa ufunguzi ulikuwa baina ya Polisi Ilemela na timu ya Tigo (picha inayofuata chini) |
Timu ya Tigo iliyoikandamiza Polisi ilemela bao 2-0 kwenye michuano ya Polisi Jamii Cup Wilaya ya Ilemela dimbani CCM Kirumba Mwanza. |
Mashindano ya kukimbiza kuku yalifana sana hapa mshindi akikabidhiwa zawadi nyinginezo toka kwa Kamanda wa Polisi Ilemela-Mrakibu wa polisi Debora Magiligimba.. |
Sikiliza hapa chini:-
Mchezo wa pili ulizikutanisha timu za kata ya Pasiansi (pichani) na timu ya soka ya Sangabuye ambapo Pasiansi iliibuka na ushindi wa bao 3-0. |
Timu ya kata ya Sangabuye. |
Mshambuliaji wa Sangabuye akitafuta mbinu kuitoka ngome ya Pasiansi. |
Kwa mujibu wa moja wa waratibu kwa michuano hiyo Kamanda wa Polisi Ilemela-Mrakibu wa polisi Debora Magiligimba amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuunganisha vijana pamoja, kudumisha amani, kutoa elimu juu ya ulinzi shirikishi, kusaidia vijana kupambana na uhalifu pamoja na kukomesha uhalifu ikiwemo matumizi haramu ya madawa ya kulevya hatimaye kuinua vipaji vya michezo kuwa sehemu ya ajira.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.