ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 28, 2012

DHAHABU TOKA MIKONO YA WACHIMBAJI WADOGO NGASAMO

Kupitia taarifa ya mgogoro wa WACHIMBAJI wadogo wa madini ya dhahabu Kijiji cha Igungumkilo Kata ya Ngasamo Wilayani Busega Mkoani Simiyu kupinga uamuzi wa Kamishina msaidizi wa ofisi ya madini kanda ya ziwa ya kuwataka waondoke katika maeneo wanayochimba Madini ya Dhahabu, nilikuahidi kukuonesha japo kwa ufupi video kuhusu dhahabu huu ni mwanzo tu...

Akinamama wakipondaponda mawe waliyookota pembezoni mwa mashimo ya dhahabu kwaajili ya kujipatia dhahabu ili kujikimu kimaisha. Uokotaji huu kwa wanakijiji wa hapa unaitwa 'Kuokoteza Ukware'

Picha ya jiwe lenye dhahabu...Unaona hiyo rangi ya njano au brown hivi, basi huo ndiyo mzigo wenyewe.

Dhahabu ya kwanza kabisa kibindoni.... uliza thamani yake!!!

Uhifadhi mzuri zaidi kuepuka upotevu wa hata chembe...

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.