ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 26, 2012

UKOSEFU WA HUDUMA BORA SABABU ZA WATU KUTOJIUNGA BIMA YA AFYA

Mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa NHIF, Deogratius Ntunkamazina amewaomba wadau wa afya kutumia fursa ya mikopo ya vifaa tiba na ukarabati viliyoidhinishwa na bodi ili watoe matibabu kwa uhaki.

Mkoa wa Mwanza ni miongoni mwa mikoa ambayo ina fursa nyingi za kiuchumi, kilimo, uvuvi, madini, utalii, ufugaji, na kadhalika hivyo mzunguko wa fedha ni wa kuridhisha, lakini kwa bahati mbaya watu wake hawajaonyesha mwamko wowote kuchangia matibabu kupitia mfuko wa bima wa Afya ya jamii (CHF).

Takwimu zinaonyesha kuwa hadi mwezi disemba 2011 kati ya kaya 635,723 zilizopo katika mkoa wa Mwanza ni kaya 7,213 tu zilizojiunga na CHF(asilimia 1.1)ya kaya zote.

Hivi ni viongozi wangapi mkoani Mwanza ni wanachama wa mfuko wa Afya ya jamii, kwa nini hawajajiunga? jibu ni kwamba kuna urasimu uliokithiri katika utoaji huduma za afya.

“Wagonjwa wanaotibiwa na bima katika hospitali za serikali pamoja na vituo vya afya wanaonekana wanatibiwa bure hivyo kutokupewa kipaumbele katika kupatiwa huduma”alisema Likoko.

Wanachama wameaswa kuwa walinzi wa huduma zao za afya na hasa wanapokukutana na Dawa zinazotolewa na serikali zikiuzwa katika maduka ya watu binafsi wameaswa kutoa taarifa kwa wahusika ili hatua stahiki zichukuliwe.

Wadau washiriki katia Mkutano wa Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) uliofanyika leo mkoani Mwanza.

Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo (kulia) amesema wanachama wanapofika kwenye vituo vya afya kwa ajili ya kupatiwa matibabu, watoa huduma wanatakiwa kuwaheshimu na kuwatibia mapema ili wakawahudumie wananchi wengine badala ya kuanza kusema wamefika na kadi zao.

Picha ya pamoja.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya 10 ni HUDUMA BORA ZA MATIBABU VIJIJINI NA AFYA BORA KWA WOTE.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.