ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 26, 2012

MAFUNZO YA MPIRA WA KIKAPU KWA WATOTO NA VIJANA YAFANYIKA NYAKAHOJA JIJINI MWANZA

Mafunzo ya mpira wa kikapu kwa watoto na vijana yanafanyika katika uwanja wa kanisa katoliki Nyakahoja jijini Mwanza kwa siku za jumatatu na jumatano kuanzia saa 9:00 alasiri na siku ya jumamosi kuanzia saa 2 asubuhi.Mafunzo yameandaliwa na kusimamiwa na Shirika la kijamii la Planet Social development (PSD) la jijini Mwanza pamoja na Chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Mwanza (MRBA) kupitia kamisheni ya watoto vijana na maendeleo na shule kwa kushirikiana na mlezi wa watoto na vijana (MRBA) ndg. Altaf Hirani Mansoor yakijumuisha watoto na vijana mbalimbali kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari za Jijini mwanza.Mafunzo haya yanaendeshwa na kusimamiwa na PSD na MRBA kupitia makocha na pia wachezaji wazoefu wa mchezo huu hapa mkoani Mwanza yana malengo yafuatayo.
1.Kuibua vipaji na jinsi ya kuviendeleza katika kusaidia maendeleo ya mchezo huu hapa mkoani Mwanza na Tanzania kwa ujumla ambao ni wito wa MRBA na Serikali kwa ujumla wa kutaka watoto na vijana wakishiriki katika michezo.
2.Watoto na vijana hawa wanapata nafasi ya kujenga miili yao kiakili na kimwili (mentally & physically) wanaposhiriki katika mazoezi mbalimbali.

3.Watoto na vijana hawa wanapata nafasi ya kukutana na wenzao kutoka shule mbalimbali na kujifunza mambo mbalimbali miongoni mwao.
3.Watoto na vijana hawa wanapata nafasi ya kukutana na wenzao kutoka shule mbalimbali na kujifunza mambo mbalimbali miongoni mwao.

4.Kupitia michezo watoto na vijana wanaoshiriki wanapata elimu ya jinsi ya kupata nafasi ya kwenda kusoma katika shule na vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kutakiwa kusoma na kufaulu masomo yao vizuri na pia kufanya mazoezi kwa bidii ili waweze kuwa mchezaji wazuri (scholarship program).
5.Kutoa nafasi kwa mashirika mengine ya kijamii ambayo hujishugulisha na utoaji wa elimu ya makuzi kwa watoto na vijana na kuwaelimisha katika kuzifahamu haki za mtoto katika kujifunza.

6.Kutoa nafasi kwa walimu wa michezo kuwatambua wanafunzi wao ili waweze kuwatumia katika kuunda timu za shule katika mashindano ya shule katika ngazi za kata, wilaya, mkoa na taifa (umitashumta na umisseta).
7.Kutoa nafasi kwa makocha wa mchezo huu hapa mwanza katika kujifunza namna ya kuendesha mafunzo kama haya kwa timu zao katika maeneo mbalimbali hapa mkoani.

8.Kuendeleza mafunzo ya mpira wa kikapu tuliyoyaanzisha hapa jijini Mwanza October 2011 kwa kushirikiana na Mambo Basketball kutoka Dar es Salaam yaliyokuwa na lengo la kuwatayarisha vijana kwa ajili ya kambi ya mafunzo ya mpira wa kikapu itakayofanyika mwezi wa june 2012 kwa kushirikiana na kocha wa Basketball program ya Memorial Newfound University kutoka Canada .

9.Kuendeleza na kutekeleza mafunzo tuliyojifunza wakati tulipohudhuria mafunzo ya ukocha wa mpira wa kikapu kwa watoto na vijana nchini Marekani mwaka 2009 kama US Sports program Alumni yaliyogharamiwa na Ubalozi wa Marekani – Tanzania kupitia US Sports program.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.