ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 1, 2011

KWAHERI MWANA HABARI MKONGWE DAVID WAKATI

Mtangazaji wa siku nyingi nchini Tanzania na mwasisi wa Shirika la Utangazaji la Tanganyika Broardcasting Cooparation (TBC) enzi hizo na Mkurugenzi wa kwanza mzawa wa Radio Tanzania Dar es salaam (RTD) Mzee David Wakati amefariki dunia alfajiri ya wa kuamkia leo jijini Dar-es-salaam katika hospitali ya Regency iliyopo maeneo ya Upanga,imefahamika.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa kutoka kwa ndugu wa karibu wa Mzee Wakati, mtangazaji huyo mkongwe, amefariki kutokana na maradhi ya kiarusi ambayo amekuwa akisumbuliwa nayo tangu mwaka jana. Mungu aiweke roho ya marehemu David Wakati mahali pema peponi AMEN


Marehemu David Wakati(wa kwanza kushoto) akiwa na waandishi na wanahabari wengine Ikulu jijini Dar-es-salaam walipokwenda kumuaga Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipotangaza kustaafu mwaka 1985.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.