ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 1, 2011

MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI MKOANI MWANZA

Maandamano ya wadau wanaojishughulisha na mapambano ya kudhibiti UKIMWI katika jiji la Mwanza yakiingia katika uwanja wa Nyamagana asubuhi hii.

Siku hii inatukumbusha kama sehemu ya jamii kupanga mikakati endelevu ya kuzuia Maambukizi mapya, kuzuia Unyanyapaa na kukabiliana na vifo vitokanavyo na UKIMWI.

"Kiwango cha maambukizi katika jiji la Mwanza kimeshuka toka 12% mwaka 1999 hadi 5.7% mwaka 2007 hii ni kutokana na ushirikiano wa dhati kati ya Halmashauri ya jiji na wadau wake" Ilisema sehemu ya risala toka kwa wadau wanaojihusisha na masuala ua Ukimwi katika maadhimisho siku ya Ukimwi duniani desemba mosi 2011.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Said Amanzi (shati la kitenge) akiwa na diwani wa kata ya Nyamagana Biku Khotecha kwenye Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
"Tathmini mbalimbali zinaonyesha kuwa bado kuna mianya ya mtu kuambukizwa VVU katika jamii kupitia ngono zembe na mtu aliyeambukizwa na VVU.

Sababu nyingine ni pamoja na mila na Desturi za kurithi wajane, Ulevi wa kupindukia na Umaskini kwa hiyo ili kupiga vita maambukizi mapya ya VVU mambo haya hayana budi kupigwa vita kwa gharama yoyote ile" amesema Mh. Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Said Amanzi.


Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu inayosema 'Tanzania bila maambukizi mapya, Unyanyapaa na vifo vitokanavyo na ukimwi inawezekana' imelenga kuwahimiza wananchi kupima kwa hiari ili kujua afya zao na kwa wale watakaokutwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi basi waweze kuzingatia ushauri wa KITAALAMU hii itachangia katika kupunguza vifo vitokanavyo na UKIMWI.

Hata hivyo pamoja na Halmashauri ya jiji la Mwanza kujitahidi kukusanya asasi mbalimbali katika viwanja hivyo huku ikitumia raslimali fedha zinazopatikana toka kwa wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi, maadhimisho hayo hapa jijini kwa mwaka huu hayakuwa na mahudhurio ya kuridhisha kama miaka mingine, kiasi cha kuonekana kama asasi hizo zilikusanyika kupeana ujumbe wao kwa wao bila wananchi ambao ndiyo walengwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.