ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 24, 2011

JK ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MAPADRI WALIOFARIKI KWA AJALI YA GARI RUVU PWANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa mkuu wa shirika la Makapuchini nchini Padri Wolphcan Peter kufuatia vifo vya mapadre wanne wa shirika hilo.

Mapadri hao wamepoteza maisha kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea juzi katika eneo la Ruvu mkoani Pwani.

Rais Kikwete amesema kuwa serikali iko pamoja na waumini wa shirika hilo katika wakati huu wa huzuni.

Ameongeza kuwa amesikitishwa na vifo vya mapadri hao na kuwaombea kwa mwenyezi Mungu aziweke pema peponi roho za marehemu.

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. Jamani ni masikitiko makubwa sana Mungu nakuomba uzipumzishe roho za marehemu mahala pema amina.

    ReplyDelete
  2. inalilah wainalilah rajeun

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.