ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 23, 2011

BUGANDO KUADHIMISHA MIAKA 40 YA HUDUMA KWA TAFRIJA YA KUCHANGISHA FEDHA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO/ZIMWI LA OKSIJENI BADO LIPO KIMTINDO

Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza inakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazo changiwa na uchakavu wa miundombinu uhaba wa majengo vitendea kazi na rasilimali watu.

Hayo yameelezwa leo na mkurugenzi wa hospitali hiyo Dr. Charles Majinge wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya mipango ya maadhimisho ya miaka arobaini ya tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo.

Miongoni mwa changamoto hizo ni kuharibika kwa mara kwa mara kwa mashine za X-Ray uchakavu wa mashine ya CT Scan na upungufu wa nyenzo zinazo hitajika katika upasuaji wa moyo na ubongo.
Mr Majinge amezitaja changamoto nyingine kuwa ni upungufu wa watumishi hususani Madaktari na wauguzi, kuharibika kwa mtambo wa kuchomea taka na kushindwa kuendesha tafiti za tiba kutokana na uhaba wa majengo na vifaa.

Amesema Hospitali hiyo inatarajia kuchangisha fedha desemba pili mwaka huu kutoka kwa wadau wa sekta ya afya ili kukabiliana na changamoto hizo.

Kwa takribani miezi mitatu iliyopita hospitali hiyo imekumbwa na tatizo kubwa la uhaba wa gas aina ya oksijeni hali iliyosababisha kukwama kwa zoezi la ufanyaji operesheni hata kusababisha watu kadhaa wakiwemo watoto kupoteza uhai.

Sababu za hali hiyo zinatajwa kuwa ni deni iliyokuwa ikidaiwa hospitali hiyo na kiwanda cha kuzalisha gesi hiyo nchini.

Kwa sasa kupitia ufadhili wa wizara ya afya umesaidia kwa kiasi kurejesha hali ya kawaida ya huduma ya upasuaji hospitalini hapo ingawa kuna changamoto ya kiwanda cha kuzalisha gesi ya oksijeni kurejea katika uzalishaji kwa viwango visivyokidhi mahitaji.Bugando kwa sasa ni Hospitali ya Rufaa ya juu inayohudumia wakazi wa Kanda ya Ziwa na Magharibi mwa Tanzania ikijumuisha mikoa ya Mwanza, Kagera, Shinyanga, Mara, Tabora na Kigoma, ambayo ina idadi ya watu zaidi ya milioni 14 ambao ni zaidi ya 1/3 ya watu wote wa Tanzania.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.