



WATU watatu wamefariki Dunia huku wengine wanne wakijeruhiwa vibaya baada ya gari kubwa la mafuta Kampuni ya DELBIT, lenye namba T 269 BRQ kuacha njia na kugonga magari mengine saba yaliyokuwa kwenye foleni zikitokea Buguruni kuelekea Ubungo.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, RPC CHARLES KENYELA, amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa saba mchana katika barabara ya Mandela eneo la River Side, Jijini Dar es salaam na chanzo chake ni mwendo kasi wa lori la mafuta lililokuwa likitokea Ubungo Mataa kuelekea Buguruni.
Aidha kwa upande wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari la mafuta alipojaribu kukwepa watu waliokuwa kwenye kituo cha daladala eneo la River Side na kuhamia upande wa pili wa barabara na kisha kuyagonga magari hayo.
Chanzo www.theeastafrica.blogspot.com
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.