ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 13, 2011

TOTO AFRICANS YARAMBA DUME

Timu ya Toto Africans ya jijini Mwanza leo imeingia mkataba maalum wenye jumla ya thamani ya shilingi za kitanzania milioni 48 wenye nia ya kuboresha soka lake na Jarida maalum la kimichezo la 4:4:2 Jarida la Mabingwa ambalo litakuwa likitolewa mara moja kwa mwezi likiandika na kutangaza habari za michezo za ndani ya nchi na zile za kimataifa.

Timu ya Toto katika udhamini huo imepatiwa jezi mpya, track 40 na jaketi zake, bips 30 kwaajili ya mazoezi pia timu hiyo itanufaika kupewa kurasa mbili kutoka katika jarida la 4:4:2 zitakazokuwa na thamani ya Sh.32, 400,000 katika kipindi cha miezi 12, mipira 12 yenye thamani ya Sh.250,000 na Sh. 500,000 kwa ajili ya kuwawezesha waandishi wa habari.

Mkurugenzi msaidizi wa Jarida la 4,4,2 Mutanin Yangwe akitia saini mkataba huo wenye jumla ya thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 48 kwa timu ya Toto Africans.

Katibu mkuu wa timu ya Toto Africans Salum Kaguna akitia saini mkataba huo wenye jumla ya thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 48 kwa timu ya Toto Africans.

Mikataba ikidhihirishwa kwa Wandishi wa Habari.

Viongozi wa timu ya Toto Africans pamoja na wadau wa Jarida la 4:4:2 wakipitia kurasa moja baada ya nyingine kwa mfano wa chapisho la kwanza la gazeti hilo la Mabingwa lenye mikakati ya kuinua na kukuza soka la Toto, Mwanza na Nchi kwa ujumla.


Mambo mengine ambayo Toto itanufaika nayo kupitia mkataba huo ni pamoja na kupata ufadhili wa Sh. Milioni 7 zitakazoiwezesha kulipia kodi za nyumba kwa wachezaji wake, katika kipindi cha miezi 12 ambapo upangaji huo kwa mujibu wa Yangwe utakuwa ni wa kuanzia Agosti 15 mwaka huu.

4:4:2 CREW.
“Niwashukuru sana wenzetu hawa kutoka 4:4:2 magazine ambao kweli wameonyesha moyo wa upendo kuamua kuja kutusaidia, hii ni faraja kubwa kwetu, ikizingatiwa kuwa tulikuwa na hali mbaya, na sisi tutawahakikishia kuwa tutawapa ushirikiano ili kuhakikisha kuwa timu yetu inafanya vizuri katika mechi zinazokuja za ligi kuu na nitumie fursa hii kuwaomba wanamichezo na wafadhili wengine waige mfano huu wa wenzetu ili waisaidie timu yetu”,alisema katibu mkuu wa Toto Africans Salum Kaguna.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.