ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 10, 2011

BAROW AKABIDHIWA RASMI VIATU NA SIRRO JEH! VITAMTOSHA VITAMPWAYA AU VITAMBANA??

Kamanda Liberatus Barow akizungumza na wandishi wa habari Mwanza mara baada ya kutambulishwa na aliyekuwa kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Simon Sirro.

Kamanda Barow ameahidi kusimamia suala la maadili katika jeshi la polisi, kuhakikisha wale anaowaongoza wanafuata sheria bila kushurutishwa akisema: "Na Baada ya kutoa kibanzi nitakwenda kutoa boriti nje ya jeshi la polisi kwani siwezi kubaki na boriti kibanzi kiko nje nitapanmbana na kibanzi kuisafisha nchi"

Fredrick Katulanda nae akachangia "Tafadhali usafishaji wa jeshi la polisi uwe wa dhati kwani tunaposema nyumba yenu ni chafu huku uvunguni kunatakataka na panya waliokufa juzi ugomvi ndipo unapoanza na hapo ndipo ushirikiano kati ya jeshi la polisi na waandishi unapotoweka na kugeuka kuwa uadui.....baadhi ya maafisa wanapanda vyeo mara 3,3 wengine ambao ni watendaji kazi wazuri kwa miaka sasa hola..wako pale pale kunanini au tuseme kubebana?.."

"Mimi bado nina mashaka makubwa juu ya uelewa wa watendaji wa jeshi la polisi na hasa suala linalolalamikiwa kila kukicha suala la maadili, jeshi la polisi lina mikakati gani kwa watendaji wake?" akaongeza; "Bangi, madawa ya kulevya aina mbalimbali, pombe haramu vyote vinapenya mahabusu jeh! polisi hawahusiki na hili?"

Aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Mwanza mpiganaji, Simon Sirro (kushoto) sasa anakwenda makao makuu ya jeshi la Polisi nchini kushika nafasi ya Venance Tossi kuendesha kikosi cha Oparesheni Maalum.
"Nitahakikisha divai ya zamani haiendi kwenye viriba vipya maana vitapasuka bali nitahakikisha divai mpya inakaa kwenye viriba vipya na yazamani viriba vya zamani."By Kamanda Barow.

Sehemu C' ya Waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali nchini walio hudhuria utambulisho huo uliofanyika kwenye chumba cha mikutano ofisi za makao makuu ya jeshi la polisi mkoani Mwanza.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Hapa mie naona vitampwaya tu hakuna zaidi, labda ngoje tuone kama ujambazi haujarudi kwa kasi kama enzi za mzee JR!

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.