Tangu mlipuko huo kuzuka, bakteria hiyo ime wauwa watu 22 na kupelekea takriban watu wengine 2000 kulazwa hosipitalini.
Wataalam kuhusu maambukizi ya maradhi wamegundua kuwa bakteria hiyo ya E.coli ilitokea katika shamba moja la mimea inayoota kusini mwa mji wa Hamburg.
Waziri mmoja ameliambia shirika la habari la AP kuwa bakteria hiyo imetokana na maharagwe yanayochipuza.
Waziri wa kilimo katika jimbo la Lower Saxony, mojawapo ya maeneo yaliyoathirika pakubwa na mlipuko huo amesema kuwa uchunguzi uliofanywa haukubaini moja kwa moja kwamba bakteria hiyo ilitokea katika maharagwe hayo lakini akaongeza kuwa dalili zote zinaashiria kuwa maharagwe ndio chanzo cha maambukizi na wala sio nyanya na matango kama ilivyokuwa iikidhaniwa.
Amesema jimbo lake limetuma ujumbe wa kuwatahadharisha watu dhidi ya kula maharagwe hayo.
Uvumbuzi huo huenda ukaiaibisha zaidi serikali ya Ujerumani kwa kuwa maafisa wake walikuwa wameelekezea kidole cha lawama mashamba ya Uhispania wakati tatizo lilitokea nchini humo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.