ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 6, 2011

UZALENDO WA PROF. LIPUMBA AFIKA KITUO KIKUU CHA POLISI JIJINI DAR KUJUA HATMA YA MH. MBOWE

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba juzi alifika Kituo cha Polisi Kati na kulaani kitendo cha kukamtwa kwa Mbowe akisema kinadidimiza demokrasia nchini.Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiingia kituo cha polisi cha Centre jijini Dar es Salaam majira ya mchana kufuatilia hatma ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Freeman Mbowe.

Lipumba alisema chama chake kina mpango wa kuitisha maandamano makubwa kupinga kitendo cha kukamatwa Mbunge wa Viti Maalumu wa chama hicho, Magdalena Sakaya.

Alisema Mbowe hakusitahili kukamtwa kwa sababu yuko kwenye maandalizi ya hoja za upinzani bungeni kuhusu bajeti.


Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari nje ya Kituo cha Polisi cha Centre jijini Dar es salaam mchana huu kuhusu sakata la kukamtwa kwa kiongozi wa upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ambaye bado anashikiliwa na jeshi.

“Nimeshtuka kwa sababu huyo ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na kipindi hiki ni kipindi cha maandalizi ya bajeti naye anapaswa kuwa katika kazi ya kutunga hoja kwa sababu yuko kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge,” alisema Lipumba.

Alisema kumweka Mbowe katika misukosuko ni kuminya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini.Lipumba alielezea kushangazwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda kukaa kimya kuhusu vitendo hivyo na kusema alitarajia kutolea tamko.

Wanachama na mashabiki hao wa Chadema walidai kwamba kitendo cha kukamatwa kwa kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni ni mpango uliobuniwa na CCM wa kubinya demokrasia ya vyama vingi nchini.

Mbowe na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Zitto Kabwe walikamatwa katika maeneo tofauti nchini juzi. Wakati Mbowe alidaiwa kutotii amri ya mahakama, Zitto alidaiwa kuzidisha muda wakati wa kuhutubia mkutano wa hadhara mkoani Singida.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.