ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, May 29, 2011

WATU 13 WAFARIKI DUNIA KWENYE AJALI YA BASI LA SUMRY

Watu 13 na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali ya basi la Sumry lenya namba za usajili T 646 BCT, iliyotokea jana usiku eneo la Igawa wilayani Mbarali mkoani Mbeya.

Akizungumza na wanahabari mchana huu Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amesema mpaka sasa maiti 13 wamepokelewa katika hospitali za rufaa za Mbalali na Ilembuka ambako kwa sasa wamehifadhiwa kutokana na kuwepo kwa vifaa vya kutunzia maiti.

Askari wa usalama barabarani akiangalia matairi ya basi hilo.

Dereva wa basi hilo Makame Juma ni mmoja kati ya waliofariki dunia na chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa ni kupasuka kwa tairi la mbela la basi hilo wakati likiwa katika mwendo kasi ndipo dereva akashindwa kulimudu likapinduka.

Mpaka sasa maiti zilizotambuliwa ni pamoja na Dereva huyo wa Basi hilo Makame Juma, Abiria Frolence Kitaule ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Ubaruku-Mbarali, Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Mzumbe Thomas Mchalo, ingawa pia taarifa zaidi zinaonyesha kondakta wa basi hilo pia ametambulika kupoteza maisha kutokana na sare za basi la sumry alizovaa ambazo maiti yake imekutwa nazo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.