ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 24, 2011

NI MADRID TENA KATIKA MSIMU WA DHAHABU WA SERENGETI FIESTA SOKA BONANZA MWANZA

Nikama msimu wa makombe kwao hatimaye timu ya mashabiki wa klabu ya Real Madrid ya Mwanza imeibuka washindi katika michuano wa tamasha la msimu wa dhahabu na Serengeti Fiesta Soka Bonanza lillowakutanisha mashabiki wa vilabu vinane vya soka barani ulaya mara baada ya kuwagagadua Chelsea katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye dimba la CCM Kirumba Mwanza.

Washindi wa pili Chelsea moja kati ya timu zilizo onyesha kandanda safi la ufundi wakiongozwa na rais wao Dj Cutter aliyebeba kombe.

Golikipa huyu wa Real alionyesha umahiri sana kulilinda lango lake na hii ilikuwa ni moja ya michomo ya hatari ya penati dhidi ya mabingwa hawa katika game za kuvutia za msimu wa dhahabu na Serengeti Fiesta soka Bonanza jijini Mwanza.

Kama kuna penati ilipigwa kwa ufundi na ustadi basi ilikuwa hii ya mchezaji mahiri wa timu ya chelsea mashabiki aitwaye Hussein ambaye yu mmoja kati ya wachezaji walioifikisha timu yake fainali.

M-blogishaji maarufu nchini Tanzania wa blogu ya JIACHIE 'Michuzi junior' jicho kikazi zaidi katikati ya raha na wadau wa Mwanza kulia Muhksin Mambo wa THE BIG TOP TEN na kushoto ni Ramadhani wa Vila park.

Ikafika zamu ya mashabiki kushindana kuona nani mwenye mzuka zaidi baina ya timu tajwa nane za michuano ya Serengeti Fiesta Soka Bonanza "Hayaaa twendeee!!!.."

Dakika sifuri wala halikuwa tena suala la kujificha kwani kama ni shangwe za mashabiki basi Arsenal ndiyo waliongoza kwani walijipanga bwana! kuna huyu mdau waliye mpachika jina 'TUMBO' alikuwa kivutio kweli kwa kuliongoza jahazi la mashabiki wa timu ya Arsenal katika mashangweZZz!

Shabiki wa Man U' toka chuo cha SAUTI akizungumza na Alex Luambano wa Sports Extra juu ya timu yake kuingia mitini katika kipute cha mwisho kukamilisha ungwe ya kwanza ya ligi ya mtoano dhidi ya timu ya Mahsbiki wa Inter Milan.

Nilivutiwa sana na fasi hii ya watoto wa frendZ waliojitokeza kushuhudia michuano hii ya 2011 nami nikaamua kugonga japo picha moja nao.

Mchezo wa Ac Milan na Liverpool ulioisha kwa liva kutolewa kwenye mikwaju ya penati huku kivutio zaidi akiwa mwanadada Hamisa Athumani wa Liverpool aliyesimama kishujaa katikati ya wanaume akicheza soka la kuchachafya.

Huyu ndiye mwanadada pekee aliyeshiriki michuano hii Hamisa Athumani wa timu ya mashabiki Liva (kushoto) akiwa na shabiki wa Arsenal.

Macho kwenye game mie na Humphrey Simon.

Rais wa liverpool God Mapesa akichagiza wachezaji wake kupata ushindi.

Hureeee!!!.. Michezo ni furaha! bwawa la maini mashabiki.

Kama ilivyokuwa kwa Dar es salaam kwa timu za 'mashetani wekundu' kukutana na 'vijana wa darajani' kupangwa kundi moja ndivyo ilivyokuwa jijini Mwanza, wababe hawa walikutana na matokeo kuwa ushindi kwa Chelsea.

Mara baada ya michuano kuisha meneja wa kinywaji cha Serengeti Premium Lager Alan Chonjo alwapongeza na kuwashukuru wakazi wa jiji la Mwanza walio mashabiki wa vilabu vya soka ulaya kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki Bonanza la msimu wa dhababu wa Serengeti Premium Lager iliyoshinda tuzo za dhahabu za viwango vya ubora kwa upikaji duniani yaani DLG ya Ujerumani na Monde selection ya Ubelgiji.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.