Kupitia sababu hizo na nyingine nyingi za kiusalama na kepuka mfumuko wa bei ya vyakula kijijini na nauli kwa vyombo vya usafiri Kamati yake imekuja na utaratibu mpya utakaofuatwa na watu wote ili kupunguza kadhia iliyopo na msongamano huo.
Aidha bwana Abbas Kandoro amesema kuwa serikali imeamua kuunda vituo vya kanda vilivyopewa majukumu ya
-Ukaguzi wa magari ambapo malori na magari ya wazi yamepigwa marufuku kuelekea Samunge.
-Utoaji wa namba za magari kwa kila kanda kuwa na rangi yake maalum, Kanda ya ziwa - Nyekundu, Kanda ya Kaskazini - Njano na Kanda ya Kati - Kijani.
-Ukaguzi wa wasafiri kutoka nje ya nchi
-Utoaji wa leseni za muda/ vibali maalum
-Kuangalia wagonjwa mahututi
-Kutolewa kwa matibabu ya dharura
-Usalama wa vituo na
-Kupanga muda wa kuondoka
Amezitaja kanda tatu zilizoundwa za uthibiti wa usafirishaji wa abiria kuelekea Loliondo ambazo ni Kanda ya ziwa vituo vikiwa Musoma , Bunda, Mugumu na Loliondo/ Wasso,huku njia ya Ndabaga ikipigwa marufuku, Kanda ya Kaskazini ambayo itahusisha mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Pwani Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Zanzibar na nchi jirani huku vituo vilichoainishwa vikitajwa kuwa ni Arusha mjini – viwanja vya NMC, Loliondo na Mto wa Mbu.
Wadau wa vyombo vya usafiri katika mkutano huo.
Kanda nyingine iliyotajwa ni Kanda ya Kati ikihusisha mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Manyara na Nyanda za juu kusini nacho kituo kikiainishwa kuwa ni babati.
Taarifa hiyo imewataja wasimamizi wakuu wa kanda kwa utawala kuwa watakuwa Wakuu wa mikoa ile hali utekelezaji utasimamiwa na RPC, RIO, RMO, JWTZ, TAKUKURU, RSO, SUMATRA, TRA na TANROADS.
Wakati huo huo taarifa kutoka kijiji cha Bulima katika wilaya ya Magu mkoani Mwanza zinasema kuwa kikombe kingine kimeibuliwa na mtu anayejiita SHANGAZI (Marieta Charles) ambaye ameibuka akitoa tiba ya dawa ya miti shamba yakunywa vikombe viwili kwa gharama ya shilingi 1000.
USAFIRI TOKA ARUSHA KWENDA LOLIONDO KWA BABU PEMBEZONI MWA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID.
Serikali ilisitisha safari kwenda kijijini Samunge kwa muda wa wiki moja kuanzia jumamosi ya tarehe 26/03/2011 hadi tarehe 01/04/2011 kwa magari yote hii ikiwa ni pamoja na magari ya serikali na viongozi wa aina zote, usafiri kwa njia ya ndege na Helkopta, sababu kuu zikitajwa kuwa ni hali tete za Afya, mazingira na huduma muhimu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.