Majonzi na simanzi vilitawala jana ndani ya mji wa Mwanza eneo la Kabuholo lililoko Kirumba, wakati wa kuuaga mwili na hatimaye kwenye mazishi ya kijana Jofrey Malelo(34) ambaye aliuawa kwa kupigwa na silaha yenye makali, alfajiri ya alhamisi, tarehe 20.jan.2011 tukio linalotajwa kufanywa na watu ambao bado hawajatajwa rasmi huku baadhi wakishikiliwa na jeshi la polisi, uchunguzi ukiendelea.Mama wa marehemu akilia kwa majonzi mbele ya mwili wa mwanae.
Ilikuwa ni wakati mgumu zaidi pindi ilipofika zamu ya watoto Lisa na Ronaldo (katikati) katika kutoa heshima ya mwisho kwa mwili wa marehemu baba yao, Jofrey Malelo. Pichani anaonekana pia Jack Fish (mwenye t-shirt nyeusi) ambaye ni kaka wa marehemu.
Mh.Diwani Stanslaus Mabula wa kata ya Mkolani naye akiuaga mwili wa marehemu Malelo.
Bazir Mbakile naye alifika eneo la tukio kushiriki safari ya mwisho ya Malelo. Pichani akiuaga mwili wa marehemu.
Majonzi kwa wana ndugu.
Mtangazaji wa redio Passion, Firbert Kabago wakati akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Malelo ambaye alikuwa rafiki yake wa dhati tangu shule.
Si marafiki tu bali hata ndugu kutoka mbali, mathalani hawa waliosafiri toka Wilayani Ukerewe ili wapate tu kushiriki safari ya mwisho ya mpendwa wao (aliyejulikana zaidi kwa jina Malelo).
Majirani nao walishindwa kujizuia.
Idadi ya watu waliohudhuria ibada ya mazishi ilikuwa ni kubwa sana.
Marehemu Jofrey Malelo amezikwa katika makaburi ya Kitangili Ilemela mkoani Mwanza. Nao polisi wanaendelea na uchunguzi kujua nini kisa na mkasa kwa mauaji hayo ya kinyama ya kijana Jofrey Malelo, taarifa zaidi zitakapotolewa utazipata hapa hapa kwenye blog ya jamii.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
RAIS SAMIA AFTURISHA WATOTO KIKOMBO DODOMA
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.
Mwanaidi Ali Khamis akigawa iftar kwa mmoja ya mtoto anayelelewa katka
Makao ...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.