ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 4, 2010

WENJE ALITIKISA JIJI LA MWANZA.

HABARI ZA KUREJESHWA ULINGONI KWA MGOMBEA WA CHADEMA KATIKA JIMBO LA NYAMAGANA ZIMEONEKANA KUWAGUSA WATU WENGI NA KUWA GUMZO KATIKA KILA KONA YA JIJI LA MWANZA

SASA WAPIGA KURA WA JIMBO HILO NAO WATAKUWA NA SANDUKU LA UBUNGE VITUONI OCTOBA 31, BAADA YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUTENGUA UAMUZI WA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI WA JIMBO HILO BW. WILSON KABWE ULIOKUWA UMEMPA USHINDI WA MEZANI WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI BW LAWRENCE KEGO MASHA(40).

MASHA TOKA CCM ALIPATA USHINDI HUO BAADA YA KABWE KUKUBALI PINGAMIZI LAKE DHIDI YA MPINZANI WAKE PEKEE EZEKIEL DIBOGO WENJE (32) WA CHADEMA .

BAADA YA MUDA WA WAGOMBEA KUREJESHA FOMU KWA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI KUMALIZIKA NA MUDA WA KUWEKA PINGAMIZI KUWADIA BW MASHA AMBAYE WIZARA YAKE NDIYO YENYE DHAMANA YA MASUALA YA URAIA ALIMWEKEA PINGAMIZI WENJE AKIDAI KUWA HAKUWA RAIA WA TANZANIA


KWA MUJIBU WA SHERIA ZA UHAMIAJI WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI NDIYE MWENYE UWEZO WA KUMPA AU KUMNYANG’ANYA MTU URAIA WA TANZANIA. HALI ILIYOTAFSIRIWA NA MGOMBEA HUYO WA CHADEMA KAMA KWAMBA MGOMBEA HUYO WA CCM ALIKUWA AMEAMUA KUTUMIA MAMLAKA YAKE YA UWAZIRI KUMVUA URAIA NA HIVYO KUMUONDOA KWENYE UGOMBEA, NDIPO BW. WENJE ALIPOAMUA KUKATA RUFAA KWENYE TUME YA UCHAGUZI KUDAI HAKI YAKE YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBONI NYAMAGANA .

BW. WENJE ALIZALIWA OCTOBER 2, 1978 WILAYANI ROLYA KATIKA MKOA WA MARA NA VIONGOZI NA WAZEE WA KATA YA MKOMA WILAYANI HUMO WALITHIBITISHA KUWA KIJANA HUYON NI MZAWA WA KATA HIYO NA NI RAIA HALISI WA TANZANIA.

ALIPOKUWA AKIHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI KWENYE UWANJA WA CCM KIRUMBA HIVI KARIBUNI DR. KIKWETE ALISEMA ALIMTAMBULISHA BW. MASHA ALIKUWA AMEPITA BILA KUPINGWA “BAADA YA MPINZANI WAKE KUJICHANGANYA MWENYEWE” HALI INAYOTAFSIRIWA NA WENGI KUWA RAIS HAKUWA AMEELEZWA VIZURI KUHUSU NAMNA HASA MGOMBEA HUYO WA CHADEMA ALIVYOKUWA AMEENGULIWA KWA KUTUMIA RUNGU LA URAIA.

KILA LA KHERI KWA WAGOMBEA WOTE WAWILI TUKUTANE OCTOBER 31 2010.

Tupe maoni yako

3 comments:

  1. Big up Weje, walitaka kukuchinjia ziwani wabaya watu. Karibu uwanja wa furahisha uweke wazi jinsi Masha alivyotumia madaraka yake vibaya.

    Uncleeeeeee!

    ReplyDelete
  2. ebana mungu si mwanamalundi wala si mzee masha ? mi nacho ona kijana wenje acheze ma masha dakika tisi sikiisha aongeze sit za nyongeza ? majbu tiari katyapata masha sie ndo ajila yake hilo amelisahau baada ya kulewa madaraka mtu hajawahi hata kupiga gwaride hata kushika short gun hajui anapewa wizara nyeti kama ile . ALIKUWA ANAINGIA OFISI ZA MAMBO YA NDANI ANAPIGIWA SARUTI MWAZO WA GETI HADI KWNYE KITI KOOO 2SILAUMU MJOMBA ALISAHAU KAMA KUNA NYAMAGANA AMBAYO ND AJIRA YAKE

    ReplyDelete
  3. walimu pia wanataka msaada wako kijan maake jiji hapajatuluia

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.