ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 16, 2026

YANGA SC YAACHANA NA KOCHA MSAIDIZI, YAAJIRI MWINGINE NAYE MRENO

 


KLABU ya Yanga imempa mkono wa kwaheri Kocha wake Maaidizi, Filipe Duarte da Silva Pedro baada ya  miezi miwili na ushei tangu awasili na nafasi yake inachukuliwa na Mreno mwingine, Marques Pereira Da Silva.

Filipe Pedro aliwasili Yanga kwa pamoja na Kocha Mkuu, Mreno mwenzake, Pedro Valdemar Soares Gonçalves Oktoba 25 mwaka jana.

Ni uamuzi wa ghafla unaokuja siku chache baada ya Yanga kutwaa Kombe la Mapinduzi wakiiifuga Azam FC kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 0-0 Jumanne Januari 13 Uwanja wa Gombani, Pemba.

Taarifa mbili za Yanga zimeambatana jioni hii — kuondoka kwa Pedro na ujio wa Da Silva ambaye ni Msaidizi wa pili pamoja na Mmalawi, Patrick Mabedi ambaye yupo hata kabla ya ujio wa Kocha Mkuu, Pedro Gonçalves.  
Da Silva

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment