ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 13, 2026

YANGA BINGWA MAPINDUZI CUP 2026

 


FULL TIME MAPINDUZI CUP 

Penalty imeamua matokea Azam Fc 4 - 5 Yanga Sc 

Okelo Mechi 0 Kombe 1

TIMU ya Yanga SC imefanikiwa kutwaa Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Azam FC kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 jioni ya leo Uwanja wa Gombani, Pemba. 


Shujaa wa Yanga SC leo ni mlindamlango, Abdultwalib Mshery aliyeokoa penalti ya beki wa kati raia wa Ivory Coast, Ahoutou Angenor Landry Zouzou.


Waliofunga penalti za Yanga ni washambuliaji Emmanuel Mwanengo, Mzimbabwe Prince Dube, viungo Pacome Zouzoua, Mudathir Yahya na beki na Nahodha, Bakari Nondo Mwamnyeto. 


Waliofunga penalti za Azam FC ni kiungo, Yahya Zayd, beki Twalib Nuru, kiungo raia wa Mali, Sadio Kanoute na mshambuliaji Ngita Kamanya.


Yanga ingeweza kuondoka na ushindi mapema tu kama kiungo wake Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua amgefunga penalti dakika ya 115, lakini ikaokolewa na kipa Aishi Salum Manula.


Aidha, Yanga SC pia ilishindwa kutumia mwanya wa Azam FC kucheza pungufu tangu dakika ya 55  baada ya winga wa Kimataifa wa Mali, Cheickna Diakité kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment