𝗛𝗔𝗧𝗜𝗠𝗔𝗬𝗘 ile kiu na ndoto ya kuitembelea Tanzania imetimia kwa mwanahabari wa michezo na shabiki sugu wa klabu ya Manchester City ya nchini Uingereza, Braydon Bent..
Akiwa katika ziara ya kitalii ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, picha na video za Braydon zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii, zikimuonesha akifurahia kwa karibu vivutio mbalimbali vya wanyamapori pamoja na mandhari ya kuvutia yanayoburudisha macho na kuigusa roho.
.
Katika safari hiyo, Braydon ameambatana na rafiki yake wa muda mrefu na mwalimu wake wa lugha ya Kiswahili, ambaye pia ni mwanahabari na mtangazaji wa kujitegemea, John Jackson maarufu kama JJ. @johnjackson_jj
.
Kupitia ujumbe aliouandika kwenye mitandao yake ya kijamii, Braydon aliandika:-
“LIONS 🦁 & HOT AIR BALLOON IN SERENGETI 🎈🇹🇿
ASANTE SERENGETI ☀️
SERENGETI NI NOMA! 🇹🇿
DAY 2 @serengeti_national_park”
.
Safari hiyo imeendelea kuonesha jinsi Tanzania inavyoendelea kuwa kivutio kikubwa cha utalii wa kimataifa, huku Serengeti ikiendelea kuthibitisha hadhi yake kama moja ya hifadhi bora zaidi duniani.
.
📸 Captures by @infocusstudio.tz
CC: @braydonbentpage
#visittanzani
#visitzanzibar
Tupe maoni yako
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
0 comments:
Post a Comment