ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 11, 2026

MISRI YAWAVUA UBINGWA IVORY COAST NA KUTINGA NUSU FAINALI AFCON

 

TIMU ya Misri imefanikiwa kwenda Nusu Fainali Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya mabingwa watetezi, Ivory Coast usiku wa jana Uwanja wa Adrar mjini Agadir nchini Morocco. 

Mabao ya Mafarao jana yamefungwa na mshambuliaji, Omar Khaled Mohamed Abdelsalam Marmoush wa Manchester City dakika ya nne, beki Ramy Hisham Abdel Aziz Mostafa Rabia wa Al Ain ya Falme za Kiarabu (UAE) dakika ya 32 na kiungo mshambuliaji, Mohamed Salah anayekiputa Liverpool dakika ya 52.

Kwa upande wao mabingwa wa Fainali za 2023 nyumbani, Ivory Coast mabao yao yalifungwa na beki wa kushoto wa Zamalek,  Ahmed Mohamed Abou El Fotouh Mohamed aliyejifunga dakika ya 40 na beki wa kulia wa Strasbourg ya Ufaransa alikozaliwa dakika ya 73.

Kwa matokeo hayo, Misri itakutana na Senegal katika Nusu Fainali Jumatano ya Januari 14 kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Tangier Grand mjini Tangier, wakati Nusu Fainali nyingine wenyeji, Morocco watamenyana na Nigeria siku hiyo hiyo kuanzia Saa 4:00 usiku Uwanja wa Prince Moulay Abdellah Jijini Rabat.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment