ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 28, 2025

YANGA SC NA MTIHANI MWINGINE KESHO DHIDI YA SINGIDA BLACK STARS

 

UONGOZI wa Yanga SC umeweka wazi kuwa unalitaka kombe lao la CRDB Federation Cup kwa kuwa wao ni watetezi licha ya kukutana na timu ngumu fainali. 

Kesho Juni 29 2025 Yanga SC itacheza na Singida Black Stars mchezo wa fainali.

Yanga SC imetoka kutwaa taji la 31 la Ligi Kuu Bara kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba SC. Ni pointi 82 imefikisha ikifunga jumla ya mabao 83 ikiwa ni timu namba moja kwenye kufunga mabao mengi na kufungwa mabao machache ambayo ni 10.

Simba SC imepishana na mataji yote ambayo ilikuwa inapambania na iliondolewa hatua ya nusu fainali na Singida Black Stars kwenye CRDB Federation Cup.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema wanatambua ushindani ni mkubwa na fainali ya Jumapili Zanzibar haitakuwa nyepesi.

“Singida Black Stars walitusumbua kweli kwenye mechi zetu mbili za ligi. Kuelekea kweye mchezo wetu wa fainali tupo tayari na tunalitaka kombe letu licha ya ugumu ambao upo mbele yetu. Tunaamini benchi la ufundi na wachezaji watakamilisha majukumu yao.”

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment