ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 7, 2025

PACOME AFUNGA BAO PEKEE YANGA YAILAZA COASTAL UNION 1-0 MWENGE

 


MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee leo, kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua kwa kichwa dakika ya 34 akimalizia krosi iliyochongwa na Max Nzengeli aliyepokea pande toka kwa beki Israel Patrick Mwenda kutoka upande wa kulia.

Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 64 katika mchezo wa 24 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi saba zaidi ya watani wao, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi.

Kwa upande wao Coastal Union baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 25 za mechi 25 sasa nafasi ya 13 kwenye Ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka daraja.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.