Dar es Salaam. Mwenyikiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amegomea kesi yake ya kuchapisha taarifa za uongo kwa njia ya mtandao wa Youtube kusikilizwa kwa njia ya video na badala yake anataka kesi hiyo isikilizwe kwa njia ya wazi.
Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi, Aprili 24, 2025 na askari magereza mwenye nyota tatu, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa mara ya pili kusikilizwa kwa njia ya mtandao.
Askari huyo wa Magereza ambaye hakujitambulisha jina lake, ametoa taarifa hiyo kwa njia ya video akiwa mahabusu.
Awali, wakili wa Serikali Mwandamizi, Job Mrema ameieleza Mahakama hiyo kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa hoja za awali na upande wa mashtaka upo tayari, ila mshtakiwa hayupo mahakama hapo.
Mrema ametoa maelezo hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Geoffrey Mhini.
Kutokana na maelezo hayo, upande wa utetezi umepinga upande wa mashtaka kumsomea hoja za awali mteja wao kwa njia ya video na badala yake wanataka mshtakiwa apelekwe mahakamani kama sheria inavyoelekeza.
Wakili wa utetezi, Peter Kibatala amepinga Lissu kusomewa PH kwa njia ya video kwa madai kuwa sheria iko wazi anatakiwa kuletwa mahakamani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.