NA ALBERT GSENGO/MWANZA
"Ndugu zangu naomba msaada wa fedha za matibabu au kupata bima ya matibabu ili nipate kuondokana na maumivu haya ninayoyapata sasa, natanani siku moja niishi na familia kama wanaume wengine, kwani sijawahi kuonja raha ya kuwa mwanaume yaani baba" "Niko tayari hata kutibiwa kwa bondi (mkopo) ili nikishapatiwa matibabu na kupona nipatiwe kazi au kibarua ambacho kitafidia fedha za matibabu yangu" Hizi ni baadhi tu ya kauli zilizojaa simanzi za kijana asiyejuwa kesho yake itakuwa vipi, Daudi Jegi Lusanja mwenye umri wa miaka 21 mwenye tatizo la njia ya haja ndogo akikojoa kwa msaada wa mpira uliounganishwa moja kwa moja kutoka kwenye kibofu chake cha mkojo mara baada ya kupata ajali ya kuangukiwa na kifusi cha mawe kwenye mgodi wa wachimbaji wadogo (kabla ya mwekezaji) uliopo kijiji cha Dutwa wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu nchini Tanzania. Akitembea taratibu kwa kujikongoja na kuzungumza kwa shida bila uchangamfu Daudi Lusanya anasema ajali hiyo ilimpata mwaka 2021 na sasa yapata miaka mitatu akiwa anakojoa kwa shida. Ameomba wasamaria wema, makampuni, vikundi na watu wa kada zozote kumsaidia kuondokana na changamoto kubwa aliyonayo inayomsababisha kushindwa kufanya kazi zoyote kumwezesha kupata kipato na kuendesha maisha. Kwa msaada na kumtumia fedha za matibabu wasiliana naye kupitia simu namba +255 680 408 335 Jina litakalojitokeza ni Willy Mwapili.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.