MABINGWA watetezi, Yanga SC wamefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 8-1 dhidi ya Stand United jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Nyota wa mchezo wa leo ni kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso aliyehusika kwenye mabao saba kwa kusaidia upatikanaji mabao matatu na yeye mwenyewe kufunga manne.Alifunga mabao yake dakika za 10,48, 58 na 61 huku pia akiwasetia beki Nickson Kibabage kufunga dakika ya 20 na kiungo Mzambia, Clatous Chama mawili, dakika ya 32 na 40.
Bao la nane la Yanga liliparikana kwa ushirika wa wachezaji waliotokea benchi, mshambuliaji Mzambia - Kennedy Musonda akifunga kwa kumalizia krosi ya kiungo Farid Mussa, huku bao pekee la Stand United likifungwa na Msenda Senda dakika ya 48.
Yanga sasa itakutana na JKT Tanzania ambayo jana iliitoa Pamba Jiji FC ya Mwanza kwa kuichapa mabao 3-1 Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
Nusu Fainali itazikutanisha Simba SC iliyoitoa Mbeya City kwa kuichapa mabao 3-1 juzi hapo hapo Uwanja wa KMC na Singida Black Stars iliyoitoa Kagera Sugar kwa kuifunga mabao 2-0 Uwanja wa CCM LITI mjini Singida jana.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.