Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda, Jeannine Mukandayisenga dakika ya 49 akimchambua kipa wa Kimataifa wa Kenya, Winfrida Seda Ouko.
Kwa ushindi huo, Yanga Princess inafikisha pointi 27, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi saba na vinara, Simba Queens ambao pia ni mabingwa watetezi baada ya wote kucheza mechi 12.
JKT Queens ipo katikati yao, Simba Queens na Yanga Princess ikiwa na pointi 32 katika nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 12 — na kesho inacheza na Mashujaa Queens Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
KARIAKOO DERBY WANAWAKE | Goli pekee la Jeannnine Mukandayisenga dakika ya 49 limeipa Yanga ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba Queens, katika mchezo wa ligi kuu ya Wanawake, uliopigwa kwenye Dimba la KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.