ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, February 23, 2025

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA KUZINDULIWA KESHO PWANI

 


NA VICTOR MASANGU ,PWANI 

KAMPENI ya msaada wa kisheria ya mama Samia, ambayo inasimamiwa na Wzara ya katiba na Sheria, inatarajia kuanza kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi wa mkoa wa Pwani kwa siku tisa lengo likiwa ni pamoja na kutatua migogoro mbalimbali ikiwemo ya ardhi.

Akizungumza na waandishi habari Ofisini kwake  Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesema kwamba kampeni hiyo itazinduliwa siku ya kesho jumatatu ambapo itaongozwa na  jopo la wanasheria watashiriki kutoa huduma hiyo kwa wananchi katika wilaya zote za mkoa huo.

Amesema katika kampeni hiyo ambayo tayari imekwisha tolewa katika mikoa 19 na sasa wakielekeza Mkoa wa 20 inaenda kutoa elimu ya Sheria sambamba na kutoa msaada wa Kisheria kutatua migogoro mbalimbali ya wananchi.

Amesema kampeni hiyo itaanza Februari 25 na kumalizia machi 05, mwaka huu na kwamba wanasheria hao watawasaidia wananchi kuandaa nyaraka mbalimbali za kisheria.


Mbali na hilo Kunenge amewataka wananchi wenye changamoto za kisheri ikiwemo migogo ya ardhi na  ndoa kushiriki kikamilifu ili kupewa msaada huo ambao utatolewa bure bila malipo yotote.

"Gharama zote zimelipwa na serikali hivyo kilichobaki ni muitilio wa wananchi kushiriki kupata huduma niwatake  wajitokeze kwa wingi ili changamoto zao zitatuliwe na malengo ya serikali yaweze kufikiwa"alisema

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.