NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Benki ya NMB imedhihirisha tena ukubwa wake nchini, baada ya mwaka huu kuweka rekodi kwa kutwaa zaidi ya tuzo 30 zinazotambua ubora wa huduma zake, ubunifu, ufanisi katika uendeshaji na utendaji, pamoja na mchango wake mkubwa katika ujenzi wa taifa. Mafanikio hayo ya kipekee kitasnia na makubwa kitaifa na kimataifa yalibainishwa jana jijini Mwanza na Afisa Mtendaji Mkuu, Ruth Zaipuna, katika mkutano wa viongozi wakuu wa benki hiyo pamoja na mameneja wa matawi yake zaidi ya 240. Akizungumza pembezoni mwa mkutano huo, Zaipuna alisema ushindi huo ni hatua kubwa kwao inayotokana na juhudi za wafanyazi pamoja na uwekezaji unaofanyika katika teknolojia za kisasa na kubuni masuluhisho ya kuwahudumia wateja na taifa kwa ujumla. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Ng'wilabuzu Ludigija, pamoja na kuipongeza NMB kwa mafanikio makubwa inayoendelea kuyapata na kuchangia katika ujenzi wa taifa na maendeleo ya nchi kwa ujumla pia ameuambia mkutano huo kuwa uwepo wa benki hiyo katika kila eneo nchini kunaifanya kutegemewa na Watanzania karibu wote hata wale wanaoishi vijijini pamoja na viongozi wa ngazi zote kutokana na kushirikiana kwake kwa karibu na Serikali.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.