VICTOR MASANGU, PWANI
Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kimesema kwamba kimeshinda kwa kishindo na kufanikiwa kuweza kuchukua mitaa yote 146 ndani ya Mkoa mzima katika uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na kuwepo kwa ushirikiano wa kutosha baina ya viongozi pamoja na wanachama ikiwemo sambamba kutoa hamasa kuanzia ngazi za chini kuhusiana na umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupiga kura.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake katika mahojiano maalumu kuhusiana na suala zima la kumalizika kwa uchaguzi wa serikali Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Pwani Dkt. David Mramba amesema kwamba wameweza kuibuka na ushindi wa kishindo kutokana na maandalizi mazuri ambayo wameyafanya katika maeneo mbali mbali ili kuweza kushinda.
Dkt. Mramba amesema kwamba katika Mkoa mzima wa Pwani kuna jumla ya kata zipatazo 133 na kwamba wameweza kushinda kwa kishindo kikubwa katika mitaa hiyo yote ambapo wagombea wote waliogombea katika kuwania nafasi ya uenyeviti wa serikali za mitaa ushindi wote umekwenda kwa chama cha mapinduzi (CCM)
"Ndugu zangu waandishi wa habari nimeona niwajuze juu ya matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambao umemalizika Novemba 27 mwaka huu katika hali ya ulinzi na usalama na chama chetu ma mapinduiz (CCM) tumeweza kushinda kwa kishindo kikubwa sana na hii ni baada ya kunyakua mitaa yote ipatayo 146 ambayo ipo katika Mkoa wa Pwani na hii imetokana na hamasa kubwa ambayo tumeweza kuitoa kwa wanachama wetu pamoja na kuwahimiza wananchi kwa ujumla,"alifafanua Dkt. Mramba
Aidha Dkt. Mramba amefafanua kwamba katika uchagzui huo mbali na kushinda katika mitaa yote ya Mkoa wa Pwani pia katika vitongozi vyote vipatavyo 2028 wameweza kupoteza vitongoji tisa tu ambavyo vimechukuliwa na vyama pinzani kutokana na kuwepo kwa sababu mbali mbali ambazo zilikuwepo katika baadhi ya maeneo.
Kadhalika Mramba meweza kusema kuwa katika ngazi ya vijiji CCM imeweza kushinda kwa kishindo na kuweza kufanikiwa kuibuka kidedea katika vijiji vipatavyo 416 kati ya vijiji 417 ambapo kijiji kimoja kimekwenda kwa chama pinzani na kwamba kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi mwingine wa kuziba nafasi ambazo maeneo mengine haukuweza kufanyika kutokana na sababu mbali mbali.
Kadhalika Katibu Dkt. Mramba amesema kuwa Mkoa wa Pwanini moja kati ya mikoa ambayo imeweza kutenda haki zaidi ya kukiheshimisha chama cha mapinduzi (CCM) kutokana na kufanya vizuri zaidi kuanzia hatua za awali kushika nafasi ya kwanza kitaifa katika zoezi la uandikishaji wa daftari kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Katika hatua nyingine Dkt. Mramba amemshukuru kwa dhati Mwenyekiti wa (CCM) Taifa ambaye pia ni Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo ikiwa sambamba na kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo kwa wananchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.