MAKAMU wa Rais Dk Philip Mpango amesema marehemu Dk Faustine Ndugulile alikua kiongozi mwenye nidhamu, rafiki wa kila mtu na kiongozi aliyeweza kutetea vema maslahi ya Taifa.
Makamu wa Rais amesema hayo leo Novemba 30 alipofika nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika Dk Faustine Ndugulile Kigamboni jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuifariji familia pamoja na waombolezaji wote.
Makamu wa Rais amewaombea faraja na moyo wa uvumilivu wote walioguswa na msiba huo.Amewashukuru wote walioshiriki katika kuifariji familia wakati huu wa kipindi kigumu kwao na kutoa wito kwa Watanzania kuendelea kushirikiana katika nyakati mbalimbali zinazojitokeza katika jamii ikiwemo za majozi na furaha.
Aidha amesema inapaswa kuendelea kumshukuru Mungu kwa maisha ya Dk Ndugulile hapa duniani. Ameongeza kwamba ni vema kwa Watanzania kuendelea kuishi vizuri na ndugu na majirani.
Akiwa nyumbani hapo, Makamu wa Rais amesali pamoja na familia, ndugu, jamaa na marafiki kumuombea marehemu Dk Faustine Ndugulile.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.